BEKI wa timu ya Simba na timu ya Taifa Stars, Shomari Kapombe amesema kuwa anashangazwa na taarifa zinazosambaa kwamba amejitonesha kidonda jambo ambalo halina ukweli wowote.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kapombe amesma kuwa alikuwa akifanya mazoezi binafsi kutokana na programu ambayo ameachiwa na kocha wa timu ya Simba.
"Nimepewa programu maalumu na kocha wa Simba, ambayo itachukua muda kidogo, hivyo baada ya kuitwa timu ya Taifa niliwasilisha 'proposal' yangu kwa timu ya Taifa ili wajue ukweli na wao wawe na maamuzi juu yangu kwa kuwa nilikuwa nina muda maalumu ambao sikutakiwa kugusa uwanja.
"Nimepigiwa simu na watu wangu wa nyumbani wakiwa wamepoteza furaha, wakiniuliza kwa nini sijawaambia kama nimeumia tena? Imeniumiza sana kwani hakuna ukweli wowote mimi naendelea na mazoezi na sina tatizo lolote zaidi ya kuendelea na mazoezi niliyopewa na kocha wangu wa Simba, nipo vema na ninaendelea salama," amesema Kapombe.
Kuna watu wanaomtakia maovu ndio wanaomtangazia hayo yote. Subiri Ndugu yangu Kapombe Mungu yupo nawe
ReplyDeleteTanzania kumekuwa na matumizi mabaya ya vyombo vya habari.Watu hawana adabu hata kidogo kwani mtu ana lala akiamka anazusha jambo ambalo halina ukweli wowote na kulitangaza na kuwaumiza wahusika na hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na vyombo husika mbaya zaidi hata kuombana radhi hakuna.
ReplyDeleteLakini hii imezushwa na mario ndimbo ndio alisema kapombe kaumia
ReplyDeleteHuyu huyu ndimbo juzi akiishusha kagera suga
ReplyDelete