June 14, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa wamejitokeza wachezaji zaidi ya 500 kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye kikosi hicho ambalo lilianza Juni 12 litakamilika Juni 16.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United,Cales Katemana amesema kuwa wamepokea jumla ya wachezaji 500 ambao wanafanyiwa mchujo chini ya kocha Felix Minziro kuwapata wachezaji 10.

"Tanzania kuna vipaji vikubwa na wengi wanapambana na sasa tunahitaji wachezaji 10 tu baada ya mchujo wetu kukamilika kati ya wachezaji 500 ambao wamejitokeza.

"Mpaka sasa tumefanya mchujo na tumepata orodha ya wachezaji 25 ambao kesho tutawafanyia mchujo mwingine ili kuwapata wachezaji 10 ambao wataingia moja kwa moja kwenye kikosi chetu cha Singida United," amesema Katemana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic