June 11, 2019

MWENDO Mdundo sasa kwa timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imeweka kambi nchini Misri kwa ajili ya kujiaanda na michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.

Benchi la ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu, Emmanuel Ammunike ameongezewa makocha wawili ambao wameongeza nguvu kwenye kambi hiyo na imeelezwa kuwa wamewahi kufanya kazi na Ammunike.

Makocha hao wote ni raia wa Misri wanaifanya timu hiyo kwa Sasa Stars kuwa na makocha sita, ambao kwa pamoja jukumu lao ni kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyotumwa na Ofisa Habari, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa, makocha hao wameongezwa kwa mahitaji maalumu. 

“Kocha Abdelrahman Essa amebobea katika ujuzi wa mazoezi ya viungo wakati Ali Taha yeye ni mtaalamu mwenye ubobevu wa kutathmini kiwango,” ilisema taarifa ya Ndimbo.

Ikumbukwe kuwa Stars ni timu ya kwanza kutia timu Misri ipo kundi moja na timu ya Nigeria, Kenya na Senegal.

1 COMMENTS:

  1. mwandishi utapoteza washabiki kwa style yako ya kuweka habari humu bila kuhakiki, taifa star haiko kundi moja na nigeria

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic