KUFUATIA taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo kueleza kuhusu hali ya beki wa timu ya Simba na timu ya Taifa Stars, Shomari Kapombe kwamba amejitonesha majeraha yake Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ameibuka na kuhoji kuhusu ukweli.
Ndimbo alisema kuwa wachezaji wa Stars wameanza mazoezi ambapo watafanya mazoezi kwa muda wa wiki moja kabla ya kwenda nchini Misri kwa ajili ya michuano ya Afcon na kueleza kwamba Kapombe amejitonesha Kidonda.
"Mchezaji Kapombe amejitonesha kidonda wakati akifanya mazoezi na wachezaji hivyo hajafanya mazoezi na wenzake mpaka pale hali yake iakapotengamaa," alisema Ndimbo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara alihoji kuwa hizo taarifa zimetolewa na nani na wapi ameumia mchezaji wa Simba ilihali ameachiwa program na kocha.
"Ni wapi taarifa za kuumia au kujitonesha kwa Kapombe zimetokea?. Kapombe anayo program maalum anayoifuata kwa sasa na wala hajajitonesha kokote kule,na kiukweli amesikitishwa na hizo taarifa zinazozagaa katika mitandao ya kijamii.
"Nimeongea nae na ameniomba niwaombe Wanasimba na Watanzania mzipuuze taarifa hizo zisizokuwa na chanzo (Source) Na Inshaallah Mungu atamponya kiraka huyu mwenye Mapafu makubwa na ufundi wa kutosha," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment