June 12, 2019

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa sasa ipo nchini Misri ambapo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.

Kikosi kilikuwa na jumla ya wachezaji 39 awali ambapo mchujo wa kwanza ulichuja wachezaji saba na mchuju wa pili ulichuja wachezaji 9 na kufanya wachujwe jumla ya wachezaji 16 na kufanya wabaki wachezaji 23.

Mchujo Wachezaji saba walioachwa kwenye kikosi kabla ya kukwea pipa ulikuwa namna hii

1. Ibrahim Ajibu- Yanga
2.Jonas Mkude- Simba
3.Ally Ally -KMC
4.Shomari Kapombe- Simba
5.Ayoub Lyanga- Coastal Union
6.Kenedy Wilson- Singida United
7.Kassim Khamis- Kagera Sugar

Wachezaji tisa walioachwa kutoka kwenye kikosi kilichokwea pipa mpaka kambini nchini Misri ni:-

1. Claryo Boniphace - U20.
2. Selemani Salula – Malindi FC.
3. David Mwantika - Azam FC. 
4. Abdi Banda - Baroka FC
5. Fred Tangalu - Lipuli FC.
6. Miraji Athuman – Lipuli FC.
7. Shiza Kichuya – ENPPI.
8. Shaban Chilunda - Tenerife.
9. Kelvin John – U17.




1 COMMENTS:

  1. Kwa kiasi fulani roho inaniuma. Kocha si Mungu anamapungufu yake na moja ya kosa moja kubwa alilolifanya kocha wetu wa timu ya Taifa ni kitendo cha kumtema Ibrahim Ajibu.Sio kwa ushabiki au kimapenzi bali kiufundi kwani ukikiangalia kikosi cha taifa stars utagundua hakuna midfielders zenye uwezo mkubwa wa kulisha mafowadi kama alivyo Ajibu au Abubakari sure boy au hata kichuya ila wacha tusubiri. Ajibu ni assist wa ukweli na angekuwa msaada mkubwa kwa akina Samata.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic