June 12, 2019

meelezwa kuwa uongozi wa Yanga umeamua kubadili gia angani kwa kuanza mazungumzo ya kumuogezea mkataba kiungo wao Ibrahim Ajibu ambaye mkataba wake umememalizika ndani ya Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa kwa sasa Ajibu yupo kwenye mazungumzo na Yanga ili kuona namna gani atarejea ambapo viongozi wamekuja na gia mbadala kwa kuifuata familia ya Ajibu.

Taarifa zimeeleza kwamba baada ya kuona Ajibu amegomea ofa ya ktua TP Mazembe uongozi wa Yanga ukazungumza na familia ya Ajibu ambao wao wanapenda kuona kijana wao akiwa Jangwani huku habar zikieleza tayari amelamba mkataba kwenye timu yake ya zamani Simba.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa wanajua uwezo wa Ajibu ila kwa sasa suala la mkataba wake hawawezi kulizungumzia.

2 COMMENTS:

  1. Yanga wasihangaike na Ajibu kwani hata jibu kitu ana timu tayari. Yanga kwa Ajibu sasa wamekuwa kama mwanaume asiejua kukutaliwa.Na Wasi wasi mkubwa wa Yanga ni kwamba Ajibu asiende Simba kama vile wanaushindani na Simba kwa Ajibu. Mbona Simba hawakumuekea mizengwe Ajibu alipoamua kujiunga na Yanga? Hata lile deal la Mazembe halikuwa hasa kwa manufaa ya Ajibu bali ni kwa kuikomoa Simba isimsaini Ajibu kwa kuamini kuwa Mazembe watampa maslahi makubwa zaidi kuliko Simba na Ajibu asingeweza kukataa kwenda Mazembe. Mazembe licha ya madai yao lakini nnaimani kabisa hawakuwa na haja ya Ajibu kwa umuhimu waliomtakia Samata kwani nnaimani kabisa Mazembe wanapomhitaji mchezaji kwa matakwa yao basi hakuna cha kuwazuia.kwa Ajibu kama vile Mazembe walilazimishwa kumsaini na mwisho wa siku ndio kama ilivyotokea .

    ReplyDelete
  2. mshitakiwa wewe polisi wewe hakimu wewe - wabongo bana !!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic