June 13, 2019


Imeelezwa kuwa klabu za Azam na Yanga  zimeanza kuwania saini ya mchezaji bora wa ligi kuu Zanzibar msimu 2018/19, Abdulswamad Kassim kutoka klabu ya Malindi.

Tetesi hizi zimeibuka huku wawili hao wanashiriki Ligi Kuu Bara wakiwa na nia ya kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.


Ikumbukwe Yanga na Azam hazikufanikiwa kutwaa taji la ligi msimu uliomalizika siku kadhaa zilizopita na sasa zinapambana kuweka sawa vikosi vyao.

Taarifa kutoka Malindi zinasema uongozi wa klabu hiyo hauna tatizo na unachotaka ni kufikiana mwafaka na kati ya Yanga ama Azam ili aweze kuondoka.

Kuna uwezekano mkubwa Kassim akatua Yanga kwa taarifa za ndani ambazo zimedukuliwa kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic