July 6, 2019


Lanchi ya juzi haikuwa na raha kwa mashabiki wa Yanga, baada ya Simba kumtambulisha rasmi Ibrahim Ajibu kwamba amerejea Msimbazi.

Simba imemfanyia kufuru nahodha huyo wa Yanga ambapo kila sekunde atakayokuwa akipumua hata kama atakuwa amelala nyumbani kwake watamlipa Sh116. Iko hivi dau lake la usajili alilokunjia mfukoni katika mkataba wa miaka miwili ni Sh.mil 80.

Mshahara wake kwa mwezi ni Sh.mil 5, maana yake ni kwamba kwa mwaka ataingiza Sh.Mil 60. Hiyo inamaanisha pia kwamba kila wiki kwa mshahara huo, Simba itakuwa ikimlipa Sh.Mil 1,250,000 kwa wiki, sawa na Sh 166,700 kwa siku.

Kwa mchanganuo huohuo, Ajibu atakuwa akilipwa Sh 6946 kwa kila saa ndani ya miaka miwili.

Hiyo ni nje ya posho za mechi kama timu ikishinda au kutoa sare na umateumate mwingine wa kishikaji anaopewa na mashabiki.

Mtendaji mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesisitiza kwamba wiki hii ndiyo ya mshtuko mkubwa kwenye usajili wao ingawa hajaweka wazi wanaofuatia.

4 COMMENTS:

  1. Maneno kama hayo ndio yanayowapa kiwewe jamaa kwahivo ndio uchokozi WA makusudih

    ReplyDelete
  2. Mshahara mdogo sana haulingani na mshahara atakaolipwa Aliudi Ambukile akiwa mazembe.

    ReplyDelete
  3. Tatizo si mshahara kwani katika ulimwengu wa soka la sasa mshahara wa milioni 5 na dau la mil 80 nimiongoni mwa malipo kiduchu Sana. Tatizo kujitambua mm nimwshaona dalili ya Ajibu kumaliza soka lake na hio mil 80 huenda likawa dau lake la mwisho kubwa alilolipata. Simuoni Ajibu atakaepata pesa Zaid ya hapo baada ya miaka yake miwili ya mkataba kuishi. Nachelea kusema sitashangaa kumuona Ajibu akigomea kutolewa kwa mkopo kwenda ndanda, mwadui, coastal,au hata kmc. Sitalishangaa Hilo kwani yeye mwenyewe amemua kuhangaika na timu za kariakoo ambazo hazina fadhila wala shukurani. Leo mzee akili mali anasema Ajibu alikuwa kirusi yanga, kirusi gani huyo mwenye asist 17 na goal 7? Kirusi gani huyo aliekuwa akicheza mpira wa kuvutia Tena akiwa anadai mshahara wa miezi sita? Nikweli Ajibu alikuwa kirusi? Au akili mali yeye ndio kirusi yanga? Hizi ndio kauli za wakosa shukurani hata uwafanyie Nini. Tukumbuke Ajibu alipotoka Simba haji manara aliongea porojo Kama hizi, kashfa za kumwaga lakini leo anaremba hoo karudi nyumbani, hoo aliondoka kwa amani. Hili soka letu litabaki kuwa lakisiasa Hadi lini? Yale Yale ya ccm na chadema ndio tunayaleta kwenye soka letu.maskini Ajibu bado hajitambui kuwa aliondoka Simba a akiwa ameshuka kiwango uwezo wake ulikuwa unafifia, lakini alipofika yanga ameng'aaa sasa anarudi kulekule badala kuvuka mipaka yanchi. Elimu inasaidia Sana mpira bila shule kwa sasa nikupoteza muda. Nina amini Kama vijana wetu watapata angalau shahada mojamoja tu, zitawasaidia Sana ktk soka lao.

    ReplyDelete
  4. amekataa ofa ya gari,nyumba na mshahara wa mil.8 mazembe,halafu ile ni njia ya kupaa kmataifa zaid mana ni klab inayotambulka duniani kote ktk hl amepotea kaka ye2

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic