July 4, 2019




BEKI wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba Zana Coulibary amerejea Bongo ambapo kwa sasa anakamilisha mazungumzo na mabosi wa Simba kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa msimu ujao.

Coulibary ambaye aliletwa kuwa mbadala wa Shomari Kapombe imeelezwa kuwa uwezo wake umemkosha Kocha Mkuu, Patrick Aussems na amependekeza asiachwe msimu ujao.

“Coulibary kwa sasa anakula upepo wa Dar na tayari mazungumzo yamefika sehemu nzuri hivyo muda wowote kuanza sasa atatangazwa kuwa mali ya Simba kwa kandarasi ya miaka miwili,” kilieleza chanzo hicho.

Coulibary kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kwamba amerejea Tanzania.


4 COMMENTS:

  1. Simba imesheheni na inazidi kusheheni na Kuna atayepata pressure lakini itahitaji kuvumilia na kujikaza kwasababu huwezi kuona tambarare bila ya kukwea mlima ha kujiepusha na kauli Kali na za kubeza

    ReplyDelete
  2. Nimuombe sana COLIBAL azidishe kujituma hasa wakati wa kukaba la sivyo naamini bado hana uwezo wa kucheza simba sc ya sasa na pia naona jina linakatwa kwenye dirisha dogo la usajili aje na ujio tofauti ili awe bora zaidi.

    ReplyDelete
  3. SIMBA HAWANA BENCH ZURI LA UFUNDI NA WANGEKUA NALO WASINGEWAACHA WACHEZAJI WAZURI
    1 KOTEI - 2 JUKO - 3 OKWI
    YANGA KAMA WANAYO PESA WAMCHUKUE JUKO HAWATAJUTA KWA UAMUZI HUO

    ReplyDelete
  4. Kwangu mimi hapa Simba imechemsha. Kulikuwa na umuhimu gani wa kumsajili Coulibally{international player)? Kwanini wasingetumia gharama ndogo kumsajili Salum Kimenya hasa ukizingatia kuwa Waziri amesema mwaka huu mwisho wa wachezaji kucheza wa kimataifa kwenye TPL ni watano tu? Mnazuia nafasi bure na kulipa gharama kubwa wakati ungemsajili Mtanzania kwa bei nafuu sana?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic