AMRI Said amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya Biashara United ya Mara.
Ofisa Habari wa Biashara United, Shomari Binda amesema kuwa unaamini uwezo na mbinu za Said ambaye ameinusuru timu kubaki kwenye ligi msimu ujao wa 2019-20.
"Tunaamini kwa uzoefu na mbinu alizonazo anaweza kuisaidia timu msimu ujao, kabla ya kumwaga wino tayari alishawasilisha ripoti hivyo tunaifanyia kazi ili kutimiza kile ambacho anakihitaji," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment