Nyota wa Simba Emmanuel Okwi amejiunga na timu ya Fujairah Footbal Club inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE), imeelezwa.
Okwi ambaye msimu wa 2018/19 akiwa ndani ya Simba alifunga jumla ya mabao 15 na anashikilia rekodi ya kufunga 'hat trick' nyingi kuliko wote akifunga jumla ya mbili ameshindwa kuelewana na mabosi zake Simba.
Chanzo cha habari kutoka nchini Uganda, kimeelezwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zinahitaji huduma yake ni pamoja na Simba ambao walishindwana naye kwa dau alilohitaji kuwekewa mezani huku klabu nyingine ambazo ni pamoja na Kaizer Chief ya Afrika Kusini ilitajwa kuwa miongoni mwa timu iliyokuwa inahitaji saini yake.
"Wamekubaliana, nafikiri hatarudi Simba. Inaonekana msimu huu alitaka kuondoka na kujaribu sehemu nyingine, ndio maana aliwaambia wasubiri," kilieleza.
Okwi alifanikiwa kuingoza vema timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes" hadi kucheza hatua ya 16 Bora ya Afcon nchini Misri, yeye akifunga mabao mawili.
Juhudi kubwa za Simba kumbakiza zimeonekana kukwama baada ya Mganda huyo kufanikiwa kutega mitego yake vizuri akiwasisitiza Simba kwamba atazungumza nao baada ya michuano ya Afcon.
Hata hivyo, baada ya kufanya vema katika Afcon, huku akiwa mchezaji huru, Okwi akawa na nafasi kubwa zaidi ya kusajiliwa na timu nyingine akiingiza fedha nyingi zaidi kuliko angebaki Simba.
Uganda huyo amekuwa bora uwanjani lakini mwenye akili nyingine ya kujua afanye nini inapofikia wakati wa usajili.
Mara ya kwanza aliondoka Simba akiuzwa nchini Tunisia, baadaye alirejea tena na kuuzwa nchini Denmark lakini saa ameondoka akiwa huru.
Tayari kashapotea huyo akirudi bas tumuone kama Boban vile, nahisi angeenda Afrika angewika zaidi, sawa ila ameangalia mshiko sana, kwa sababu kama ni kipaji tayari kashakitangaza sana kwa hyo kachagua sahihi maana akitoka huko sidhani kama atakuwa na thamani tena.
ReplyDeleteSIMBA SPORTS CLUB BOSS DID NOT NOTICE EARLY ABOUT OKWI`S DEPARTURE, BUT THERE WAS 98% FOR HIM NOT SIGNING FOR SIMBA.
ReplyDeleteI don't think Okwi was suppose to leave. This is because of misunderstanding with the chief coach. Sometimes was showing not happy with the substitution.
ReplyDeleteKumzuia mchezaji asiondoke kwa namna yoyote iliyotofauti na dhmira yake ni mojawapo ya dalili za utumwa mamboleo..
ReplyDeleteKama alidhamiria kuondoka wamuache aondoke..!!
Ni yeye mwenyewe mwenye uwezo wa kuamua mustakabali wa maisha yake..!
Ni jukumu la #Simba kufanya replacement ya maana kwenye hiyo nafasi iliyoachwa wazi..!
Okwi left Simba peacefully while he was desperately needed despite repeated attempts to remain, but peacefully without insults or provocative language
ReplyDeleteYaani kaacha Simba nakuenda Fujairah.....Naona kama siamini kabisa...
ReplyDelete