‘Hata kagere na kina Okwi wajuzi waliyasema haya haya ‘
Na Haji Manara
Siku hizi sijishughulishi tena na kujibu jibu makala zenye lengo la kuichafua klabu yetu,nimeacha kwa sababu moja tu,wakosoaji wetu ni wale wale na kwangu hawana jipya sababu tushawazoea na tunawajua tabia zao za kutaka wao waonekane ndio Wajuzi zaidi wa soka kuliko Watanzania wote.
Lakini hili la upotoshwaji wa usajili wa Deo kanda nimeona nilisemee japo kidogo ili niwakumbushe Wanasimba wenzangu kuhusu kebehi za Wanazengo hao walizozitoa baada ya usajili wa Mawaria kina Meddie kagere na wenzie.
Nyote mnakumbuka kebehi na maneno ya wakosoaji wetu kabla ya msimu uliopita kuanza,waliandika Simba ni Shikamoo Jazz,timu ya wazee, haitafika kokote na maneno mengi ya kuonyesha klabu imefanya usajili wa hovyo sana,
Na tuliambiwa hata raundi ya kwanza ya ligi ya Mabingwa Afrika hatuvuki!!
Utatu wa John Boko,Emmanuel Okwi na Meddie kagere ulipondwa hadi na mikongojo, yupo mmoja aliandika Simba inajifanyia dhambi yenyewe kwa kusajili vibabu vilivyojichokea!!
Uhhh lalaaah!! Nikiwauliza baada ya msimu kuisha ni utatu upi uliokuwa bora ktk msimu uliopita wa ligi kuu kuwazidi hao wazee , sijui kama watanijibu!!
Idadi tu ya magoli waliyoyafunga msimu uliopita kwa pamoja ni rekodi isiyoguswa na washambuliaji wowote wale kabla na baada ya uhuru!!
Kagere ambae alikuwa mfano wa vibabu akawa top score wa ligi kuu, na kiukweli ndio best player wa ligi yetu ilioisha!!
Wanazengo hao wajuaji pia waliiponda sana beki yetu chini ya Pascal Wawa na Erasto Nyoni, lakini hao ndio mabeki walioruhusu magoli machache mno Kwenye ligi kuu ya msimu uliopita.
Leo watu wale wale ‘wajuaji ‘kwa nia ile ile na dhamira zao zile zile wanasema Deo kanda ni mzee na kutoa sababu zao zisizo na chembe ya ufahamu wa soka bali ujuzi wa kishabiki usioshabihiana na uhalisia wa mambo !!
Eti kanda alikuja Taifa na timu ya Congo miaka kumi iliopita hvyo hawezi kuwa na uwezo ule ule aliokuwa nao mwanzo!!
Yesu wangu!! Hv hii football tunayoiandikia tunaijua au tunaichukulia poa tu?
Miaka kumi iliyopita ndio Simba ilimsajili Emmanuel Okwi ambae bwana mjuzi kamsifu kwa kucheza vzuri Kule Misri Kwenye Afcon, lakini hapo hapo anahoji kama kanda ataweza kuwa na ubora wa kumrithi Okwi ambae alimuona miaka kumi hiyo hiyo nyuma!!
Cha kushangaza Okwi huyu huyu waliemwita mhenga leo anapambwa kwa kuonekana ni bora sana sababu anaondoka Simba!!
Hawa ndio watu wetu ambao hujui hata malengo ya maandishi yao wanayoyabatiza majina makubwa ili kuhalalisha tenzi zao!!!
Halaf anahoji why kama ana uwezo hayupo ktk team ya taifa?
Lakini hakuwahi kuhoji kuhusu kutokuwepo kwa kina Makasu uwanjani au kutoitwa kwa Makambo ambae ni mshambuliaji mwenye uwezo na umri mdogo!!
Hv hafahamu Kupata nafasi Congo Kwenye timu ya taifa ni tofauti na Uganda au Tanzania?
Anajua sana ila hapa anatupa dhamira yake kutuonyesha Simba na uongozi wake hawana wajualo ktk mpira ila yy na wenzie ndio wajuzi wa huu mchezo murua zaid duniani!!
Labda nimfahamishe yy na ww msomaji wa makala hii fupi,
Deo kanda alikuwa na ugomvi binafsi na kocha na akasema auzwe,Simba ikapeleka ofa TP Mazembe lakini Klabu hiyo ikagoma kutuuzia ila ikakubali kumleta kwetu kwa mkopo,na hii peke yake inathibitisha ubora wa Nyota huyo mwenye uzoefu mkubwa wa kusukuma gozi la Ng’ombe
Na nimjuilishe pia dua lake la eti Simba itashindwa kuanzia pale ilipoishia msimu uliopita litaishia juu ya Dari, tumesajili kwa ufundi na mapendekezo ya benchi letu la ufundi na pia kwa kuzingatia matakwa na matarajio ya klabu Kwenye msimu ujao wa ligi,
Klabu yetu haisajili kwa presha ya ‘Wachambuzi ‘inasajili kwa matakwa yetu na kwa ushauri wa wataalamu kweli wa soka,ndio maana kinatoka kitu ( Okwi) kinakuja kitu ( Kanda)
Nimalizie kwa kuwaambia wajuzi hiki sio kipindi cha kutuvuruga na kuwachanganya Washabiki wetu ambao tunajitahidi kuwahenga henga ,so hatutakaa kimya kwa yoyote yule ambae tunadhani anataka kutugombanisha uongozi wa klabu na Wanachama pamoja na Washabiki wetu!!
Endeleeni kumjadili Haji,klabu yetu iacheni,Simba haiwezi kuchezewa chezewa kwa kisingizio cha uhuru wa mawazo, na ikiwa hvyo mkubali mawazo yenu kupingwa hadharani!!
Leo umesema vema.
ReplyDeleteSi amtaje tu aache mafumbo kama muimba taarabu .Anajibu kichoandikwa Jicho la mwewe.
ReplyDeleteHaji Tanzania tulipewa uhuru kupita kiasi lakin ninachokijua hawa wanaiponda simba ndo wa kwanza kuandika simba hii sasa sifa yampa mtu saba
ReplyDeleteKHaji umeongea.Kwanza kweli watu wanakumisi siku nyingi hujasikika.Najua bado una majonzi ya Taifa stars kwani wewe licha ya kupewa ulaji na mshika mpini Makonda lakini kamwe hukuacha kueleza hisia zako za wazi kabisa juu ya uwezo wa aliekuwa kuwa kocha wa Taifa stars Amunike. Manara tunajua bado kamati ya saidia Taifa stars ingali hai na wewe ni miongoni mwa wajumbe muhimu kabisa wa kamati hiyo. Na hapana shaka Manara una access au ufikio wa haraka wa aiza mwenyekiti wako Makonda au Raisi wa TFF. Ujumbe ni kwamba, kwa kutumia nafasi yako sasa wadau tunajua akiteuliwa kocha wa hovyo wa Taifa stars basi tunajua Manara kahusika labda tuone umejiuzulu kutoka nafasi yako ya mwenyekiti wa hasira ya maendeleo zidi ya Taifa stars. Tunachojua kamati ya ushindi ya Taifa stars imejaa wajumbe weledi kabisa kunako mpira. Na ushindi siku zote huanzia kunako uteuzi wa makocha bora.Taifa stars ilifungwa tangu siku ya mwanzo alipoteuliwa Amunike kuwa kocha wake mkuu..Manara unaujua mpira na makocha kwa hivyo kwa kutumia nafasi yako hakikisha Taifa stars inapata kocha bora na wenye vigezo. Hata Tanzania tulisema ilishashindikana kwa rushwa na mambo mengine ya hovyo ila kocha Magufuli kaja kupindua meza na Tanzania sasa ni habari nyengine Africa na Dunia. Taifa stars haijashinda bado ila bado hajapatikana kocha wa ukweli. Na siku akipatikana kocha wa ukweli basi siku yake ya kwanza ya kuanza kazi watu wote watajua kuwa kocha keshapatikana wa kukata mzizi wa fatina. Tunahitaji kocha wa viwango taifa stars na bila hilo watu wakome kuwalaumu wachezaji.Asante.
ReplyDeleteUlipo kosea ni kumuingiza muuaji kwenye issue hii huku ukimsifia.
DeleteKwanza kabisa Simba walifanaya jitihada kubwa tu ya kumbakisha Okwii na nadhani Okwii angeshaondoka zamani sana pale simba kama si jitihada za viongozi wa Simba kumbakisha.Lakini Okwii mwenyewe nadhani kaamua kutaka kuondoka simba na wakati mwengine hata kiwango anachoonyesha akiwa Simba anacheza kana kwamba analazimishwa sasa nadhani kwa mchezaji ikishafika hali kama hiyo ni vizuri kumuacha mchezaji aondoke kwani kuendelea kumbembeleza ni kujaribu kumueka mchezaji husika kuwa juu ya klabu. Ila Deo Kanda ni mchezaji mzuri zaidi ya Okwii na kwa mazingira ya Simba Deo Kanda atang'ara zaidi akiwa Simba. Tungewashauri viongozi wa Simba wapambane hivi sasa kummiliki Deo Kanda kuwa mali yao mapema. Kanda Kuwa mchezaji wa mkopo kutoka kwa Mazembe ni janja na kamtego wa Mazembe wa kuja kuwapiga simba zaidi kihagrama pindi Kanda akichanganya. Kanda ni mchezaji mkubwa sidhani Simba kama watakuja kuiweza vita yakuja kumbakisha hapo baadae kutoka kwa timu zenye nguvu ya pesa zaidi. Usirikiano wa Kanda na kagere hawa watu wana nguvu na kuujua mpira vilivyo na sioni beki yeyote ya timu pinzani ya kuwazuia hawa watu ligi kuu. Simba wanahitaji kumkabidhi Kanda mkataba wa miaka mitatu to be honest tena wanatakiwa kufight au kulishughulikia hilo suala sasa bila ya kuchelewa.
ReplyDelete