July 10, 2019


GADIEL Michael, bieki mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga amewaomba radhi viongozi wa Yanga na mashabiki wake.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Michael ameandika namna hii:-
"Wakati mwingine mtu unalazimika kufanya maamuzi yako peke yako kwa sababu anaewajibika na maisha yako mwisho wa siku ni mtu mwenyewe.

 "Mpira ndio kazi yangu ya kimaisha, maamuzi niliyoyafanya yalikuwa ni muhimu sasa kwa maslahi yangu na familia yangu.

"Nimuombe radhi aliyekuwa meneja wangu Jemedari Saidi Kazumari kutokana na sintofahamu iliyotokea kwa kutomshirikisha nikiamini asingekubali nihame mtaa.

 "Nimelazimika kufanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana yangu mwenyewe na familia yangu.

 "Kikubwa ni kwamba Mpira ni familia moja, bado tuko kwenye familia,hakuna chuki maisha yaendelee.

"Niwashukuru wanaYanga wote kwa ushirikiano walionipatia, nilikuwa na furaha sana kwao. Pia niwashukuru viongozi wa Yanga chini ya mzee Msolla. Mimi ni mwanadamu, kiumbe dhaifu, Maana aliekamilika ni Mola wetu pekee. Nawaomba radhi sana," amemaliza Michael.

10 COMMENTS:

  1. Kwani kuhama timu dhambi? Unatafuta maslahi bhana

    ReplyDelete
  2. Mwanaume kasema kama mm niliyesoma nimeguswa basi wakupe baraka maana hatujui maisha yako na majukumu uliyonayo isiwe chuki kakiwashe kwa aman kamanda. Hata kama watakubagua na kukuchukia basi mlango wa mbinguni hawakai wao

    ReplyDelete
  3. Ungekuwawa muazi mapema Nani angekulaumu we nenda zako

    ReplyDelete
  4. Huo ni uungwana kuliko Yule anaye tema ghadhabu pale mmoja anapojiamulia kutafuta maisha mema kwengine Jambo ambalo halitokei kabisa katika nchi zilizostaaraibika kimpira Kama vile akina Samata ns Msuvi walipojiamulia au pale walipohamia Ajibu na Yondani na wengine wengi kuelekea Yanga wakati ule kutafuta maisha bora

    ReplyDelete
  5. Gadiel....hongera kwa uungwana..nmepend hapo kwenye kusema maamuz ya maish yako yanaamuliwa na ww mwemyew

    ReplyDelete
  6. Mimi nimekuelewa vizuri na nimependa nasaha zako ila mapungufu madogo yaliyotia doa ni kutokuwa muwazi tangu mapema kwani kama ulivyosema "anaewajibika na maisha yako mwisho wa siku ni mtu mwenyewe" sidhani kama ungetoa tamko mapema angetokea mtu wa kukuzuia kwenda unapotaka.Kila kheri maana kiangazi daima hakipigi upande mmoja,hutokea wakati mwingine ukame ukahamia kanda nyingine.Awamu hii ni zamu yetu kupambana na ukame lakini tutakunywa hata maji ya tope na ya kwenye vidimbwi ilimradi maisha yasonge mbele."MV MAPENZI MELI YA WAPENDANAO,BENDERA INAPEPEA SAFARI YAENDELEA"

    ReplyDelete
  7. Usingeomba msamaha nafikir ungewashukuru tyu. Maana hata pindi unaenda Yanga kuna team Ilikua inakuhitaj na wakakosa huduma yako. Katafute changamoto ingine

    ReplyDelete
  8. Nenda zako,hakuna anayekuhitaji.Samahani haisaidii kitu kwa wakati huu

    ReplyDelete
  9. Kumbuka ulipotoka Azam ulitoka kwa sarakasi na kwa tabia hiyo wewe kwenye soka mafanikio utayasikia tuu.nenda zako huko na hata yanga ulikuja baada ya deal la simba kubuma ukajikuta kule Azam ulishaharibu,nadhani wewe ulikuwa mamruki yanga kwani hakuna asiyejua habari zako

    ReplyDelete
  10. Ondoka tu Afcon ulikuwa chujio la nazi, hata ungebaki ungecheza nafasi ipi? maana kila idara imekamilika huku. Waulize kina niyonzima kilicho wakuta huko kwa Mikia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic