July 23, 2019


NYOTA wa Nkana FC ya Zambia, Walter Bwalya amejiunga na timu ya El Gouna FC ya nchini Misri.

Bwalya alikuwa anatajwa kuwindwa na Simba ili kuziba pengo la Emmanuel Okwi ambaye hajaongezewa mkataba ndani ya kikosi hicho ambacho kimeweka kambi nchini Afrika Kusini.

Amesaini kandarasi ya miaka mitatu kwa dau linalotajwa kuwa na thamani ya dola 650,00 sawa na bilioni 1.4 za kitanzania.

1 COMMENTS:

  1. Dollar laki sita na elfu hamsini? Sio mchezo ila watanzania bado tumelala kwani mpira unalipa lakini tunawaacha vijana wetu wazembee.Mfano Simba kwa level waliofikia sasa wana uwezo wa kukuza na kuuza akina Bwalya wengi wa nje na ndani ya nchi na klabu ikafaidika zaidi na huko ndiko kutajairika. Kwa bahati mbaya Okwii kaandoka kama mchezaji huru ila Simba ilistahiki kufaidika na mauzo ya Okwii. Nasaha tu kwa uongozi wa Simba najua kuna watu makini pale simba wakiongozwa na Mo ni kwamba Simba licha ya kuwa na malengo ya kufika mbali Africa lakini vile vile wafikirie zaidi jinsi ya kunufaika na biashara ya wachezaji. Tumejifunza kutoka kwa Justin chonga wa Orlando pirates na sasa Bwalya na kabla ya hapo Makasu aliekuwa wa As vita na hata kwa kagere ni kwamba mchezaji mwenye uwezo wa kweli na hasa kama atakuwa ana umri mdogo akienziwa kulinda kipaji chake basi kila siku zinavyosogea mbele na ndivyo thamani yake inavyosogea juu vile vile. Kuulekea klabu bingwa Africa nawashauri Simba kwa roho safi kabisa kama watakuwa hawajaiziba hiyo nafasi moja ya mchezaji wa kigeni basi lazima watafute mchezaji wa malengo atakaeweza kuja kuisaidia Simba kimpira na kibiashara na katika miongoni mchezaji nnaopendekeza Simba kutofanya utani kumsaini basi ni Mganda wa KCC PATRIC KADU kama jina nimelipatia sawa sawa huyu ni zaidi ya Bwalya kama utamfuatilia na kuna uwezekano wa kufanya makubwa zaidi na akawa biashara ya mamilioni baadae na msaada kwa timu ila wanamchezaji mwengine bora zaidi sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic