GADIEL MICHAEL AIBUA JINGINE LA KUSHANGAZA YANGA, SIMBA WATAJWA
Inadaiwa kuwa beki wa Yanga, Gadiel Michael juzi jioni amesaini rasmi mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Gadiel amesaini mkataba huo wa kukipiga Simba ni baada ya mvutano wa muda mrefu kati yake na mwajili wake wa zamani Yanga katika dau la usajli ambalo ni Shilingi Milioni 60 alizokuwa anazihitaji.
Beki huyo anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Yanga kusajiliwa na Simba ni baada ya kipa Beno Kakolanya na Ibrahim Ajibu kusaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.
Meneja wa mchezaji huyo, Jemedari Said alisema kuwa hana taarifa za beki huyo kusajiliwa na Simba baada ya mawasiliano kati yake na beki wake kupotea kabla ya jana jioni kumpikia simu.
Jemedari alisema kuwa beki huyo amempigia simu baada ya kuona taarifa kwenye mitandao amesaini ambazo yeye binafsi kama meneja wa mchezaji huyo zimemshtua.
Aliongeza kuwa, kama beki huyo atakuwa amesaini mkataba Simba atashangaa kwani Yanga ndiyo ilikuwa klabu yake ya kufanya mazungumzo na kuwaahidi viongozi anabakia tena Yanga kitendo ambacho kitakuwa kimkera kama kweli amesaini Msimbazi.
“Mimi kwangu Gadiel kama mwanangu kwa jinsi nilikuwa ninaishi naye na mimi ndiyo niliyempeleka Azam FC na baadaye Yanga tena baada ya Simba kumkataa wakati ninampeleka.
“Nilimpeleka Simba yeye akiwa na akina Bocco (John), Nyoni (Erasto) na Manula (Aishi) nikiwa kama meneja, lakini cha kushangaza timu hiyo ya Simba ilimkataa kwa kusema kuwa wanaye Tshabalala (Mohammed Hussein).
“Baada ya kukatiliwa Simba nikampeleka Yanga nikashukuru wakampokea na kumfanya hivi sasa kuwa katika kiwango cha juu, sasa ninashangaa kuona akiidharau Yanga na ubaya wa hizi timu kubwa hautakiwi kuondoka vibaya.
“Ndani ya wiki hii Gadiel sikuwa na mawasiliano naye mazuri na ninaomba nijitoe kwenye hili kama kweli amesaini Simba na hii ya kusaini itakuwa na ukweli kwa sababu simuelewi huyo dogo, nitafute baadaye usiku (jana) nitakuwa na majibu mazuri kwani ninakwenda kuonana naye na ninaomba nisieleweke vibaya kwa Yanga,” alisema Jemedari.
Inauma sana, lakini ili wanajangwani tutambe msimu huu virus waondoke tu!
ReplyDeleteMm nawashauri yanga wajipange na wala wasiumie ktk hili. Kiukweli Kama Sheria za tff zingeruhusu kusajili wageni 15 basi mm ningeshauri timu zote zinazoshiriki mashindano yakimataifa zisajili wageni wengi na firs eleven ijae wageni watupu kwani hakuna mchezaji hata mmoja wa bongo anaeweza kukupa angalau asilimia 85 ya uchezaji kwenye mech za kimataifa. Kama unataka kutoka mapema kwenye mashindano nenda na hawa kina gadiel Michael sijui kaseke sijui feitoto sijui mkude, Hawa niwachekaji tu timu ikipigwa 5. Tunaipongeza simba imefika hatua ya juu mwaka Jana lakini ukitafuta utaona ni juhud binafsi za kina kotei, okwi, kagere, na chama ambae chama ndie alieipeleka Simba robo fainal. Hata lile kulubali ambalo tunaliona garasa lakini kwenye mechi za kimataifa linacheza mpira mwingi mno kuliko hao kina tshabalala mnao wasifu. Kama kweli unataka kufika mbali kimataifa, huwez lia eti umempoteza Ajibu, sijui gadiel Michael, sijui ndemla, hao ni kapeto wahapahapa tu kwenye mechi za lipuli, ndanda, mbao. Embu kumbukeni kilichowapata mtibwa kwenye cuf federation, walipigwa nje ndani Kama watoto na KCC ya Uganda, wakati hakuna anaekataa kuwa kwenye soka la ndani mtibwa Ina wachezaji bora wenye Kasi na niwazalishaj wa vipaji. Simba yanga Azam na kmc Kama kweli wanataka kupiga hatua CUF basi wajikite Zaid na wachezaj wanje nasio kwenda na kina mudathiri sijui Dante, hufiki popote. Simba mmeshakuwa na hamasa Zaid yakufika mbali basi msiwaendekeze Hawa kina gadiel hawana msaada wowote kwenye champion ship, bora mkamtafute kibatambuzi au walusimbi kuliko Hawa, mtaendelea kupigwa tano na watakaba kwa macho na mwezie akipigwa chenga yeye anacheka. Yanga msiumie na kina gadiel pokeeni hao kina bigrimana, sibomana, kalengo hayo ndio majembe ya cuf yanayo jitambua.
ReplyDeleteBado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!
ReplyDelete