July 10, 2019


Wakala wa Kiungo wa Manchester United Paul Pogba anaamini "kutafikiwa suluhisho la kuridhisha hivi karibuni kwa pande zote" katika kuamua mustakabali wa mchezaji huyo.

Ijumaa iliyopita, ajenti Mino Raiola taliliambia gazeti la The Times kuwa kiungo huyo mwenye miaka 26 anataka kuhama Manchester United.

Pogba, ambaye yupo katika ziara ya kabla ya msimu na klabu ya Man United katika nchi za Australia, Singapore na China, alisema mwezi Juni kuwa "huu unaweza ukawa muda muafaka kuhamia kwengine".

"Mchezaji (Pogba) hakufanya kosa lolote," Raiola aliuambia mtandao wa Talksport.

"Amekuwa na heshima na weledi. Klabu imekuwa ikijua hisia zake kwa muda mrefu.

"Ni aibu kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kukosoa bila ya kuwa na taarifa sahihi, na ninasikitishwa kuwa klabu haichukui hatua yoyote kwa wanaofanya hivyo."

United watacheza na Perth Glory Julai 13 na kisha Leeds United Julai 17, baada ya hapo watasafiri mpaka Singapore kwa mchezo mmoja dhidi ya Inter Milan Julai 20.

Watamaliza ziara yao ya maandalizi kwa mchezo mmoja dhidi ya Tottenham jijini Shanghai Julai 25.

Paul Pogba yupo kwenye kikosi cha Man United kilichopo kwenye ziara ya maandalizi ya msimu ujao nchini Australia.

Manchester United bado haijapokea ofa rasmi ya usajili kutoka klabu yeyote inayomtaka Pogba na uongozi upo kimya juu ya tetesi za usajili kumhusu mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 89.

Klabu za Real Madrid na Juventus tayari zimeshatangaza nia ya kutaka kumsajili Pogba. Lakini mpaka sasa hawajatuma maombi ama kukutana na uongozi wa United kufanya mazungumzo ya usajili.

Inaarifiwa kuwa Pogba amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa, lakini kiuhalisia ni mitatu sababu United waliongeza uwezekano wa kusalia mpaka 2022.

Kipengele hicho kinawapa nguvu kubwa United kwenye meza ya majadiliano endapo Real ama Juventus watawafuata.

Kwa sasa, maafisa wakuu wa United wanaonekana kuwekeza muda wao wote kwenye maandalizi ya msimu mpya na wanaamini Pogba atakuwa kwenye kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kitakachominyana na Chlsea kwenye mchezo wa kwanza wa msimu wa 2019/2020 dhidi ya Chelsea kwenye uga wa Old Trafford Agosti 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic