July 31, 2019

USIKU wa kuamkia leo klabu ya Yanga imeshusha mashine mpya kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa leo.

Mchezaji huyo ambaye ni mwili jumba inaelezwa kuwa amekuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo ambaye amejiunga na Horoya AC.

Mwinyi Zahera alisema kuwa nafasi iliyobaki ndani ya kikosi hicho ni ya mshambuliaji.

Jina lake anaitwa David Muringe ametokea klabu ya FC Lupopo pia amewahi kucheza soka la kulipwa nchini Angola msimu uliopita alitupia mabao 14 katika mechi 16 alizocheza.

11 COMMENTS:

  1. Mabao 14 katika mechi 16 ni rekodi kali sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kweli ni kali, atakuta na ndanda

      Delete
  2. lipeni kwanza akina Yondani au Dante wanaowadai.Mbona timu inakuwa dhulmat

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlipeni JUUKO MURSHID kwanza,mbona Simba ni wadhulumaji namna hiyo!

      Delete
    2. inakuhusu nini wee bwege....angalia mambo yanayokuhusu

      Delete
  3. Hata Zahera anawashangaa viongozi wake kwa jinsi wanavyowazulumu wachezaji wa zamani wenye madai yao.

    ReplyDelete
  4. Afunge magoli 14 ktk game 16 alafu Fc lupopo wamuache tu... Mmmh litakuwa bomu hili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama wale Wabrazil!!

      Delete
    2. kwa hiyo na nyinyi kipindi kile mlivyomwacha okwi aondoke kumbe lilikuwa bomu!!!!!!!!!!!!!!!

      Delete
  5. Stori hizo wadanganyeni hao kandambili wenu si angebaki Angola huko au lupopo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic