July 6, 2019

KOCHA wa kikosi cha Kagera Sugar, Meky Maxime amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kufanya usajili makini utakaowafanya walete ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Msimu wa 2018-19 Kagera Sugar ilinusurika kushuka daraja jambo lililowapa darasa la kutosha na kuwafanya wajipange sawa sawa msimu ujao.

"Kwa sasa tumejipanga na tumeanza kazi ya kufanya usajili makini ambao utatufanya tulete ushindani msimu ujao, mpaka sasa kila kitu kipo sawa nina imani tutafanya makuwa msimu ujao." amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa ndani ya Kagera Sugar ni pamoja na Evarigitius Mujwahuki kutoka Mbao FC na Hassan Isihaka kutoka Mtibwa Sugar.

3 COMMENTS:

  1. Mjichunge sio kushuka daraja tuu bali mtazama majini kwa usajili huu

    ReplyDelete
  2. Sio kuleta ushindani lakini mchukue ubingwa

    ReplyDelete
  3. Msicheze ligi kwa kupambana na Simba tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic