IMEELEZWA kuwa sababu kubwa za wachezaji kupigwa chini ndani ya Yanga ni kudai stahiki zao za muhimu ambazo wanazidai kwa muda mrefu.
Habari za ndani zimeeleza kuwa wachezaji waliosimamishwa ndani ya Yanga ambao ni pamoja na beki mkongwe, Juma Abdul pamoja na Vincent Adrew 'Dante' wanadai stahiki zake kwa muda mrefu.
Mtoa taarifa ameeleza kuwa wachezaji wamekuwa wakiahidiwa kulipwa stahiki zao kwa muda mrefu bila kupewa.
"Wanachofanyiwa wachezaji wa ndani ni propaganda, wanapewa ahadi nyingi mwisho wa siku hakuna kinachotimia jambo ambalo limewafanya wasiibuke kambini," kilieleza chanzo hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa masuala hayo hayajafika mezani kwake kwa kuwa hajaripoti kazini kutokana na matatizo ya kiafya.
Walipwe Na Swala Hilo Kweli Linaumiza Sana Ni Sawa Na Kumdai Mtu Pesa Hataki Kulipa Na Kilasiku Unamuona Anatanua Tu Yanga Wamesajili Kwa Kishindo Huku Hawataki Kuwalipa Pesa Za Usajili Baadhi Ya Wachezaji Wake
ReplyDeleteJamani mbona mambo yapo namna hivi tunaelekea wapi. Kwanini tunatia miguu yote miwili badala ya kutia mmoja kutaka kujua kina cha maji kama kinavukika au hapana. Kwanini hatutazami uwezo tuliokuwa nao kabla ya kuingia sokoni na kuvikusanya vikubwa kuliko uwezo tulionao?
ReplyDeleteMbio za sakafuni huishia ukingoni
ReplyDeleteArusi ya fahari huku huna pesa ya matumizi ya kila siku.Kupenda sifa nä kioga ndio matokeo yake hayo.Tena tubaoongozwa nä msomi.Kupanga ni kuchagua.
ReplyDeleteNi magenu mtu huponzwa kwakudai haki ya jasho lake. Wao hawakupigwa chini kama asemavyo muandishi lakini waliamuwa wenyewe kujitenga baada ya kukata tamaa ya kulipwa malimbikizo Yao na kutokuwanacho cha kuendeshea maisha. Migomo ya Yondani musimu uliopiti ulikithiri mpaka kvuliwa ukepteni na yeye mwenyewe ndie aliyeamuwa kujipiga tena Pingu ya miaka miwili na kuanza kuhomea kabla ya kuanza hata mechi moja
ReplyDeletejamani ila kihuhalisia inauma sana maana, maisha ya sasa yanaenda kasi sana sasa iweje hawa wachezaji wasipewe haki yao hata kama mtu hana thamani kwako lakini si haki kumnyanyasa najua wangekuwa wengne basi tungesema utovu wa nidhamu, lakin kwa hawa wawili ni kweli maana ni watu tunaowajua. Hv unajua kuna wachezaji wa Yanga wanacheza bila mikataba hasa hawa wazawa, Pia hv Simba wanapokuwa wanasajili na vilabu vingine wanaweka ada ya usajili kwa mikataba yao lakin unajua mchezaji hata mmoja wa Yanga ambae amesajiliwa na kwa kiasi gani tofauti na kutwambia wamesaini miaka 2 , 3 ,1 je kwa kiasi gani hapo ndo utajua weledi wa viongozi ukiwambia wanasema mkataba wa mchezaji ni siri je vilabu vingne sio siri duniani kote?
ReplyDeleteGadiel Michael aliona mbali
ReplyDeleteMti unapokatwa hutulia palepale lakini binaadamu anapokuwa hatarini upesi hukimbia na hivi ndivo ilivokuwa Kwa Gadiel na Ajib kwasababu walikwisha kuyaomja
ReplyDelete