PAULO Gomez
Dardenne mtaalamu wa tiba ya viungo ni jembe jipya la kazi ambalo limeungana na
timu ya Simba nchini Afrika Kusini ambapo wameweka kambi ya mandalizi ya msimu
ujao.
Kocha Mkuu
wa Simba, Patrick Aussem amesema kuwa ni jambo jema kumpata kocha mpya ambaye
anajua lugha zaidi ya moja jambo litakaloongeza nguvu ya mawasiliano.
“Huyu ni mtu
wa kazi na anajua lugha nyingi nina amini atakuwa mhimili mkubwa kwenye
mapambano yetu hasa kulingana na malengo yetu ambayo tumejiwekea.
“Anajua
lugha nyingi ikiwa ni pamoja na Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihispaniola na
Kiitalia kazi ya mawasiliano imepata tiba,” amesema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment