July 6, 2019


KOCHA wa timu ya Vijana ya Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni ambao wamesajiliwa na Simba wataibeba timu hiyo kimataifa ila ndani ya Ligi Kuu Bara itakuwa pasua kichwa.

Kwa sasa tayari Simba imemalizana na wachezaji wapya Sita wakigeni ambao wana uhakika wa kuonyesha makeke yao msimu ujao ikiwa ni pamoja na:-Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Tairone da Silva hawa ni raia wa Brazili, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman raia wa Sudan, Francis Kahata wa Kenya, Deo Kanda wa Congo.

“Wachezaji wakigeni wanaosajiliwa na Simba watakuwa na msaada mkubwa kwenye michuano ya kimataifa kutokana na ubora wa viwanja ambavyo watacheza pamoja na miundombinu ila kwenye ligi ya ndani watapata taabu.

“Ukweli haujifichi hasa ukizingatia ligi yetu miundombinu bado tatizo hivyo wachezaji wengi watafanya vizuri wakiwa uwanja wa Taifa ambao una hadhi ya kimataifa wakitoka mkoani itawachukua muda kuzoea mazingira, ila ni somo kwa wazawa nao wanapaswa wapambane wasibweteke,” amesema.

3 COMMENTS:

  1. Ila mnachkesha.
    Kocha was Yanga, kuzungumzia wachezaji was Simba!!!??? Wakati wao pia wamesajili kocha was Simba haongelei kabisa habari za Yanga.
    Amakweli utofauti unaonekana wazi nani mkubwa sikuhizi.

    ReplyDelete
  2. Simba malengo yao ya usajili yamelenga kimataifa zaidi.Na ligi ya ndani ni kama mazoezi kwani walisha jaribu hivyo msimu uliopita na wakafanikiwa. Kawaida ya mpira anaeujua huwa anaujua hata ukimpeleka kwenye uwanja uliolowa mafuta atacheza tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahaaaa umenifurahisha but muhim nayo kuipa nafas....hapa ndan changamot ndo muhim kutujeng zaid

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic