July 10, 2019


Imeelezwa kuwa Mganga wa tiba za asili nchini Benin, Gwedu Sakala amemuonya mshambuliaji wa Liverpool na Senegal, Sadio Mane kutocheza mechi ya leo ya robo fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya timu ya taifa ya Benin.

Mganga huyo amemuonya Mane akidai kuwa endapo akikaidi na akicheza mechi hiyo ataanguka na kufariki uwanjani.

Kauli ya Mganga huyo imeleta mshangao kwa wengi kutoka na uzito wa aina yake ambapo Sengal itakuwa inacheza dhidi ya Benin katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali.

Mechi hiyo ya aina yake inatarajiwa kupigwa huko Misri majira ya saa 1 kamili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic