July 9, 2019

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa hauna hofu na fujo za timu kubwa ambazo zinafanya usajili wa kutisha kwani wao wana kiwanda cha kutengeneza wachezaji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanatazama namna usajili unavyokwenda hawana presha.

"Sisi Mtibwa hatuna presha hata kidogo na usajili unaofanyika na timu zote, tunajiamini kutokana na uwekezaji ambao tumeufanya kwa timu yetu ya vijana.

"Tunachosubiri kwa sasa wamalize kazi yao ya usajili kisha sisi tunapandisha mashine zetu kali zinaendelea kupambana, hapa kwetu ni chuo hatuna tatizo," amesema.

Wachezaji ambao wameondoka Mtibwa Sugar kwa sasa ni pamoja na Kelvin Sabato ambaye amejiunga na Gwambina FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Ally Shomari amejiunga na Kagera Sugar na Hassan Is-Haq.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic