July 6, 2019


BAADA ya juzi Jumatano, Simba kumtangaza Ibrahim Ajibu kuwa mchezaji wao mpya, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kufunguka kuwa mshambuliaji huyo alikuwa kama kirusi katika timu yao.

Ajibu ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2017/18 akitokea Simba, msimu uliopita aliisaidia Yanga kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara huku yeye akimaliza kuwa kinara wa asisti akiwa nazo 17 na akiifungia timu yake mabao 7.

Akizungumza na Championi Ijumaa, mzee Akilimali alisema kuwa Ajibu alianza kucheza Simba, hivyo si ajabu kumuona akirudi katika timu yake hiyo lakini anafurahi kwa kuondoka kwake kwani alikuwa hana mapenzi na Yanga.

“Ajibu alianzia Simba, mimi sioni ajabu kwa yeye kurudi huko, kwanza nimefurahi kwa kuondoka kwake kwani sasa hivi Yanga tunachofanya ni kukata mti na kupanda mti, Ajibu alikuwa kama kirusi kwa Yanga kwani alikuwa anacheza lakini siyo kwa mapenzi.
“Mapenzi yake yote yalikuwa Simba, hivyo alikuwa kama kirusi kwetu, niwashauri tu Wanayanga kuwa wasisikitike kwa kuondoka kwake.

“Kitamba cha unahodha kinafaa kurejeshwa kwa Kelvin Yondani kwani ni mchezaji mzuri, mimi nilishangaa kocha (Mwinyi Zahera) alipomvua unahodha na kumpa Ajibu lakini hatukutaka kuingilia kwani tulijua mwalimu atakuwa ameona kitu,” alisema Mzee Akilimali.

6 COMMENTS:

  1. Sungura aliposhindwa kuzifikia zabibu zilizongara mtini alisema sizitaki zimeoza ndio Hali waliyokuwanayo sasa. Kila aliowakataa sasa wamekuwa maadui na kila wanaponasihiwa wasifanye hivo wanazidi na sasa wanafanya Kwa zamu. Juu ya yote hayo mnyama kimya anatelezea mbele kujijenga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe pia ukumbuke Haji Manara aliwahi sema Yanga hakuna mchezaji wa kuchezea Simba, Simba ipo level ya Al Ahli, Mazembe, Zamalek, Esperance... sasa anakula matapishi!
      Athuman Idd alipogoma kusaini Rage alisema na aende kwao akauze ndimu na ukwaju!
      Hassan Kessy alifukuzwa akiambiwa akauze genge njaa imnyooshe, aliposaini Yanga Simba wakaandika barua CAF kulalamika kwamba kassini mkataba akiwa bado anamkataba nao!
      Viongozi wetu kama sisi tulivyo tuwe na jana na kesho.

      Delete
  2. Hata huyo Yondani naye alitokea Simba kabla ya kwenda Yanga. Mzee akili acha kupumbaza akili za watu

    ReplyDelete
  3. SIZITAKI MBICHI HIZI-NDICHO ANACHOMAANINISHA HUYO MZEE

    ReplyDelete
  4. Asiye na mapenzi na YANGA yetu aondoke, timu ni kubwa kuliko wao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic