July 30, 2019

JUMA Kaseja, nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa nafasi ya kushinda kwa timu nchini Kenya ipo kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki.

Taifa Stars mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika Cameroon 2020 ililazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kenya uwanja wa Taifa mchezo wa marudio utakuwa Agosti 4 nchini Kenya.

Kaseja amesema : "Wao wameweza kupata sare kwenye ardhi ya nyumbani, basi nasi tunaweza kupata ushindi kwenye ardhi yao Kenya, makosa yetu benchi la ufundi litafanyia kazi nasi tunajipanga tukiaimini tuna nafasi ya kusonga mbele.

"Morali kwa wachezaji ni kubwa na kila mmoja anatambua kazi yake, kikubwa ni sapoti kwa mashabiki na dua," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Wakati timu ilipotajwa nilijiuliza ni timu ya taifa ya soka la ufukweni au?

    ReplyDelete
  2. Kule? Hatutoki salama,timu ipangwe kazi kazi,sio kupanga kwa kujuana

    ReplyDelete
  3. Kabisa na namuangalia John Boko kama mchezaji alieshindwa kuyafanyia kazi madhaifu yake na kuwa bora zaidi labda kwa yeye mwenyewe kuamini yakuwa yupo vizuri na wanaomsema labda wana chuki zao binafsi. Tatizo la Boko ni moja tu ni kukosa umakini anapofika golini. Na ni tatizo sugu na mara kadhaa amekuwa akiigharimu hata timu yake ya Simba kupata magoli muhimu katika mechi muhimu sema kule simba kuna watu amabao mara kadhaa husahihisha makosa yake na kuinusuru Simba katika mechi kadhaa .Boko yupo vuzuri,ana nguvu,ana kasi na stamina ila kama mtu wa mwisho wa kupasia nyavu basi hapo ndipo kwenye shida. Kwani amekuwa akipoteza nafasi kadhaa za wazi za kufunga magoli muhimu na kwa kweli kitendo hicho wakati mwengine kimekuwa kikishusha thamani ya kazi yake. Boko anatakiwa kutulia na kutumia akili zaidi badala ya nguvu anapofika golini. Afahamu yakuwa yeye ndie mbeba msalaba namba moja kuhahakisha mpira uliotuama kwenye miguu yake ndio nafasi ya mwisho kwa timu katika kujaribu kutafuta ushindi kwa hivyo anapaswa kuwa makini muda wote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic