July 11, 2019

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara  Simba wameweka wazi kwamba msimu ujao kazi yao kubwa ni kutetea ubingwa wao na kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa wana kikosi kipana na imara ambacho kinauwezo wa kushindana na wanaendelea kusajili wachezaji wasiosikika.

"Msimu uliokamilika tulitwaa kombe la Bara pamoja na kutinga hatua ya robo fainali, hivyo  msimu ujao malengo ni kutetea ubingwa wetu wa Ligi Kuu Tanzania bara na kuvuka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Tunaendelea kusajili wachezaji wenye viwango vya juu, wenye uzoefu, ambao hamjawahi kuwasikia sio kwa ajili ya kushindana kwenye ligi ya nyumbani tu bali kimataifa zaidi." amesema.

4 COMMENTS:

  1. Simba mambo yake kimyakimya bila ya kupiga kelele utashitukia tu. Mchezaji anaetaka kuihama Simba huihama Kwa Amani na kulipwa haki zake kamili bila presha su kubezana na anayejiunga hupokelewa Kwa mikono miwili

    ReplyDelete
  2. Nilitegemea kipaumbele cha uwanja wa Bunju, Kombe la FA na Mapinduzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic