STARS YAPIGWA 3-0 NA ALGERIA AFCON, SASA KUPANDA NDEGE TAYARI KUREJEA NYUMBANI
Kikosi cha Taifa Stars kimekamilisha rasmi safari ya michuano ya AFCON huko Misri kwa kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.
Katika mchezo huo wa kundi C, Stars imepokea kichapo cha tatu mfululizo baada ya kufungwa na Senegal kwa mabao 2-0 kisha Kenya kwa mabao 3-2.
Mabao ya Algeria usiku huu yamewekwa na Islam Silmani pamoja na Adam Ounas aliyeingia kambani mara mbili.
Mabao hayo yote yamefungwa kunako kipindi cha kwanza.
Ratiba inayofuata sasa ni Stars kurejea nyumbani ikiwa haijaambulia pointi hata moja huku Kenya nao watakuwa wanarejea kwao kufutia kufungwa mabao 3-0 pia na Senegal.
0 COMMENTS:
Post a Comment