TIMU ya Taifa ya Wanawake Tanzania 'Tanzanite' chini ya umri wa miaka 20 imepata mwaliko wa kushiriki michuano ya COSAFA ambayo inazishusisha timu za jumuia ya ukanda wa Afrika ya Kusini.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Tanzania, Clifford Ndimbo amesema kuwa michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 1 mpaka 11 mwaka huu nchi Afrika Kusini.
Timu shiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na zile za nchi ya Afrika Kusini ambao ni wenyeji, Zimbabwe, Swaziland, Botswana na Namibia.
Pia, Fountain Gate Sports Academy imeingia mkataba wa kudhamini soka la vijana chini ya umri wa miaka 15 ambapo wachezaji watakaa pale huku wakipatiwa elimu bora na maadili ya kimpira pamoja na malezi bora.
Wachezaji hao waliopatikana baada ya ligi ya vijana Chini ya umri wa 15 kumalizika na wale waliobora kuchaguliwa na jopo la makocha mbalimbali, hivyo watachukuliwa wote na kulewa na shule hiyo iliyopo Dodoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment