July 5, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna papara na mchezaji wa kikosi hicho Gadiel Michael ambaye amegoma kusaini ndani ya klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa Yanga imefanya usajili wa maana hivyo hawawezi kusumbuliwa na mchezaji mmoja.

"Tumefanya usajili makini msimu huu, kama mabeki tunao mtu kama All Sonso na Ally Ally hawa wote wapo vizuri kucheza nafasi yake, ila mpango wetu ni kuwa na wachezaji wawili kila upande.

"Kama ataamua kuondoka milango ipo wazi hatuna kazi ya kumbebeleza mchezaji kwani dirisha dogo ni karibu tutasajili wachezaji wengine," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Kama unajua hilo sasa kwa nini mnapaniki?,mtakieni kila la kheri Kyle aendako

    ReplyDelete
  2. Panic bado inaendelea juu ya kuomba atulie Kwa faida ya siha yake. Nini kinachoumiza ilhali mchezaji sio wenu tena kwakuwa mkataba baina yenu umemalizika na mchezaji yupo huru hamuwezi kumkalia kooni na yeye ndie WA kujiamulia mnaendelea na kauli hizo Kwa hizo nanyi hamumdai chochote. Keshasema hela mnayotaka kumpa ni ndogo hakubaliani ayo, muongezeni mpate Saini yakr

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini hata huyo Gadieli hamna kitu tuseme ule ukweli tu....magoli mengi hutokea kwake....Yanga mna bahati sana kwakuwa sasa mtaziba moja ya mapungufu ya beki mliyokuwa nayo msimu uliopita

      Delete
  3. Michuano ya CAF CL inakuja Yanga inatakiwa iwe na beki halisia mwenye kucheza #3...lazima mmtafute beki mwenye uwezo wa kucheza CAF

    ReplyDelete
  4. Lakini hata huyo Gadieli hamna kitu tuseme ule ukweli tu....magoli mengi hutokea kwake....Yanga mna bahati sana kwakuwa sasa mtaziba moja ya mapungufu ya beki mliyokuwa nayo msimu uliopita

    ReplyDelete
  5. Ebu tuacheni zungumzia habari ya huyu jamaa. Walikuwapo akina Makambo, Ngoma, Chirwa, Kessy na wengine kibao hawajaondoka na Yanga tatizo lipo wapi jamani had mapovu yanaharibu mashati ya watu? Mwenyekiti msomi Daktari Msolla alishafunga mjadala huu ebu tukubaliane naye mapovu basi.

    ReplyDelete
  6. Sasa povu ninla nini jamani ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic