July 6, 2019


Kocha wa Kenya, Sebastian Migne amekiri kwamba staa mpya wa Simba, Francis Kahata hakuwa na bahati kwenye Afcon ya msimu huu.

Migne amekiri kwamba hata kwenye mechi na Tanzania hakuwa na wakati mzuri ingawa inawezekana alipania sana. Hata kwenye mechi na Algeria mchezaji huyo alitolewa mapema baada ya kushindwa kuhimili mchezo.

Kocha huyo anasema kwamba Kahata ni miongoni mwa mastaa ambao aliwapa nafasi kubwa ya kutisha msimu huu lakini ikawa tofauti ingawa hamlaumu kwa vile soka ndivyo ilivyo na Afcon ni mashindano makubwa.

Kahata ameripotiwa kusaini mkataba na Simba akiwa nchini hapa na atakuwa akilipwa Sh 8 mil kwa mwezi.

3 COMMENTS:

  1. Wanaotaka kubeza wabeze kama walivombeza Okwi na Kagere lakini kijana keshafika

    ReplyDelete
  2. Wanaopenda kubeza wabeze kama walivombeza Okwi na Kagere lakini kijana keshaingia na atayepandisha presha apandishe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic