July 25, 2019

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kuifanya siku ya wananchi kuwa ya kipekee kuliko zote kutokana na ukubwa Yanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ndani ya Yanga, Deo Muta, amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kuipa sapoti timu ya Yanga na kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

"Tumejipanga kuifanya iwe siku ya kipekee na wiki yenyewe itakuwa na matukio mengi ya kijamii hivyo ni fursa ya mashabiki kujitokeza kwa wingi.

"Tutakwenda Zanzibar ambapo ni sehemu ya muungano wa Tanzania lengo ni kuifanya iwe siku ya tofauti," amesema.

Kilele cha siku ya wananchi itakuwa Agosti 4 uwanja wa Taifa ambapo Yanga iacheza na Kariobang Sharks mchezo wa kirafiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic