July 25, 2019

BAO la usiku lililofungwa na nyota mpya wa Mtibwa Sugar, Abdulharim Humud jana limeweka usawa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir FC.

Mchezo huu wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Chamazi ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Haruna Chanongo dakika ya tano na la pili la kusawazisha lilifungwa na Humud dakika ya 81 baada ya wapinzani wao kusawazisha bao dakika ya 42 kupitia kwa Ngabonziza Blanchard dakika ya 42 na la pili liliongezwa dakika ya 57 na Gasongo Benjamini.

Huu unakuwa ni mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na Mtibwa Sugar, Humud ameanza kuonyesha makeke yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic