July 29, 2019

TAWI la nguvu ya Buku la Yanga lenye makazi yake Mwananyamala jana limekabidhi msaada wa ukarabati wa Wodi ya Wanaume no.5 waliokuwa wakifanya kwa takribani wiki moja kuelekea kilele cha siku ya Wananchi Agosti 4,2019.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura amesema:- "Kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja,".

 Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha amewapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano.

 Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Iyagala amesema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic