July 29, 2019

JURGEN Klopp, Meneja wa Liverpool amesema kuwa msimu ujao wana kazi ngumu ya kufanya ili kuweka rekodi mpya zaidi ya msimu uliopita.

Kwa msimu wa 2018/19 Liverpool iliweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukamata nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England huku mabingwa wakiwa ni Manchester City.

Klopp amesema:"Kwa kweli inabidi tujipange kwa kiasi kikubwa msimu ujao hasa ukizingatia kwamba kutakuwa na mechi nyingi kuanzia zile za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Carabao, Kombe la FA na Klabu Bingwa Dunia,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic