August 26, 2019


BAADA ya kikosi cha Azam Complex kuitoa Fasil Kenema kwa jumla ya mabao 3-2 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa uwanja wa Chamazi sasa kitamenyana na Triangle United ya Zimbabwe kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Triangle imefuzu raundi ya kwanza baada ya kuichapa Rukinzo ya Burundi kwa matokeo ya jumla ya mabao 5-0, ikishinda nyumbani 5-0 na ugenini kutoka suluhu.


Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ni hatua ngumu waliyofikia ila watapambana kupata matokeo chanya.

"Ni kazi ngumu na hatua ngumu kwetu, tuna jukumu la kufanya kwa ajili ya kupeperusha Bendera yetu kimataifa mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

Azam FC itaanza kucheza nyumbani mechi ya kwanza itakayopigwa kati ya Septemba 13 na 15 na itarudiana na timu hiyo kati ya Septemba 27 na 29 nchini Zimbabwe.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic