August 26, 2019


Baada ya kufanya vema katika mechi iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, inaelezwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameanza kupatwa na wakati mgumu kuhusiana na nani ampange langoni mwa timu yake kati ya Farouk Shikalo na Metacha Mnata.

Kinachomuumiza Zahera hivi sasa ni kutokana na ujio wa kasi wa Mnata akiwa langoni jambo ambalo linaleta ugumu wa nani achukue namba mbili kati yake na Mnata.

Tukio la kudaka penati kwa Mnata katika mechi ya mwisho ya Yanga CAF limeonekana kumchanganya kichwa kufanya maamuzi ya nani awe kipa namba moja na nani awe mbili.

Ushidi wa Yanga dhidi ya Township Rollers umeisaidia Yanga kusonga mbele huko wapinzani wao wakiungana na Simba nje iliyotolewa na UD Songo jana.

Mnata ameisaidia Yanga ambayo sasa itakutana na Zesco ya George Lwandamina katika mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic