August 24, 2019


MCHECHETO! Ndivyo utakavyoweza ni baada ya wapinzani wa Yanga, Township Rollers kupeleka maombi kwenye Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuomba kubadilishiwa uwanja kabla ya kukataliwa.

Hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaozikutanisha Yanga na Rollers leo.

Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 kabla ya kurudiana kesho.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa walishtushwa na taarifa za uwanja uliopangwa awali kubadilishwa ambao ulipangwa Uwanja wa Taifa wa Botswana kabla ya kubadilishwa kwenda kwenye huo mwingine.

Mwakalebela alisema Rollers walitaka kuupeleka mchezo kwenye uwanja mdogo ambao Caf wameukataa kwa kuwa haukidhi vigezo vya kutumika.

Aliongeza kuwa, uamuzi huo wa Caf ni habari njema kwa Yanga kwani sasa watacheza kwenye uwanja sawa na wa Taifa, Dar ambao ulitumika kwenye mchezo wa kwanza.

“Mchezo wetu wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana kama ulivyopangwa awali ni baada ya Caf kukataa maombi yao ya kutaka kutupeleka kwenda kucheza kwenye uwanja mdogo ambao haukidhi viwango.

“Hizo ni moja ya hujuma ambazo wamezipanga kuzitumia Rollers, hiyo ni baada ya kuingia hofu ya ubora wa kikosi chetu baada ya kutuona katika mchezo wa awali tuliocheza huko nyumbani.

“Tunafahamu presha kubwa waliyokuwa nayo viongozi na benchi la ufundi, ndiyo sababu ya kutapatapa kutaka kubadili uwanja kwa kutuhofia, kikubwa niwatoe hofu Wanayanga kwa kuwaambia kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani,” alisema Mwakalebela.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic