UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa ushindi wao umebebwa na nguvu ya mashabiki ambao walijitokeza jana uwanja wa Chamazi.
Azam FC jana ilipindua meza kibabe mbele ya Fasil Kenema ya Ethiopia kwa ushindi wa mabao 3-1 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kukubali kufungwa bao 1-0 ugenini mchezo wa awali.
Mabao ya Azam FC yalifungwa na mshambuliaji mpya, Richard Djodi raia wa Ivory Coast aliyeanza kucheka na nyavu dakika ya 23 na 31 huku lile la ushindi likipachikwa na Obrey Chirwa dakika ya 58.
Baada ya mchezo huo, wapinzani hao walitimka mazima na ndege kurejea nchini Ethiopia huku Azam FC wakibaki na furaha ya ushindi ndani ya Taifa la Tanzania.
Jaffary Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa mashabiki pamoja na wadau waliojitokeza kuipa sapoti Azam FC wamewapa moyo na nguvu ya kupambana.
"Sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau imetufanya tuzidi kupambana na kuonyesha uwezo wa kweli jambo lililotupa nafasi ya kusonga mbele kimataifa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment