KIUNGO bora
wa Simba kwa msimu wa mwaka 2018/19, James Kotei ambaye kwa sasa anakipa Kaizer
Chief amesema kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kushinda mchezo wake wa leo dhidi
ya UD do Songo ya Msumbiji endapo wachezaji watakuwa na nidhamu.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kotei amesema kuwa kwa
namna Simba ilivyo na moto ikiwa uwanja wa Taifa ni nafasi ndogo kwa wapinzani wao
kupenya kirahisi.
“Nimekuwa
ndani ya Simba kwa muda mrefu, nimeona namna mashabiki ambavyo wanaipenda
kutoka moyoni timu yao na ule wingi wao namna unavyowabeba wachezaji basi
ushindi wa kwanza umejificha kwa mashabiki.
“Hakuna
kitakachowazuia Simba kushindwa kupata matokeo wakiwa Taifa, usajili wao ni
mzuri na wana wachezaji makini kama Shiboub (Sharaf), Kahata (Francis) naamini
wachezaji wakijiamini kiasi na kuwaheshimu wapinzani basi ushindi ni halali
yao,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment