MASHINDANO ya kumtafuta bingwa mpya wa
michuano ya Sprite B Ball Kings kwenye mchezo wa kikapu yamezidi kupamba moto
ambapo leo kwenye viwanja vya JMK Parks mchakato wa kutafuta timu 16 bora
ulianza.
Bingwa mtetezi Mchenga Boys tayari ameshafuzu hatua ya 16 bora na
kufanya timu 15 kutafutwa kutinga hatua ya 16 bora kwa ajili ya kuendelea
safari ya kumtafuta bingwa mpya.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Sprite B.Ball Kings, Goza Chuma amesema
kuwa mashindano ya msimu huu yamekuwa na msisimko wa kipekee kutokana na timu
nyingi kujitokeza.
“Msimu huu
timu nyingi zimejitokeza na zimeonyesha ushindani wa kweli tunatarajia kesho kuchezesha droo ya timu 16 ambazo zitapita kwenye hatua ya mtoano.
Matokeo ya leo kwa mechi za awali za mtoano ilikuwa namna hii:-Ukonga Warriors pointi 37 v Mbagala Hard Core pointi 25, Ukonga Hitmen pointi 51 v Kigamboni City pointi 21, Oysterbay pointi 50 v Obays Finest pointi 17.
Kwemye michuano hii inayoendelea viwanja vya JMK Parks hakuna kiingilio.
0 COMMENTS:
Post a Comment