UONGOZI wa
KMC , umesema kuwa bado haujaelewa sababu za wachezaji kushindwa kupata ushindi
mbele ya AS Kigali kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho
uliochezwa Ijumaa, uwanja wa Taifa.
KMC
ilihitaji ushindi wa aina yoyote mbele ya AS Kigali mwisho wa siku walipoteza
kwa kufungwa mabao 2-1 jambo lililowafungashia virago jumla michuano ya
kimataifa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde amesema kuwa hakuna jambo
ambalo wachezaji hawakutimiziwa na waliahidiwa bonasi kubwa mwisho ndoto zao zimeyeyuka.
“Inaumiza
kwa hatua ambayo tumeshia kwani maandalizi yalikuwa vizuri na wachezaji
walituahidi kufanya vizuri kwa ajili ya Taifa mwisho wa siku tumeambulia
maumivu sio kitu kizuri.
“Kwa sasa
tunaacha yote yapite kwani maisha lazima yaendelee na nguvu zetu tunazipeleka
kwenye maandalizi ya ligi tunaamini tutafanya vizuri, kazi kubwa tutaifanya
kupata matokeo chanya mbele ya Azam FC,’ amesema Binde.
Mchezo wa
kwanza wa Azam FC utakuwa Agosti 29 utakaopigwa uwanja wa Uhuru, msimu uliopita
walipokutana uwanja wa Uhuru walitoka sare ya kufungana mabao 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment