PAUL Pogba, Kiungo mshambuliaji wa Manchester United amefunguka kuwa ishu yake ya kubaguliwa kisa rangi yake kumempa nguvu ya kuwa imara.
Pogba alishambuliwa jumlajumla kwenye mitandao ya kijamii baada ya kushindwa kufunga penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves.
Mchezo huo uliokuwa wa pili kwao ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 siku ya Jumatatu.
Pia Jumamosi, nyota mwingine wa United, Marcus Rashford alikosa Penalti Uwanja wa Old Trafford wakati wakikubali kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Craystal Palace.
Pogba amesema: "Ndugu zangu na kizazi changu kilichopita kilipambana kwa ajili ya kuleta Uhuru kwenye kazi, mabasi pamoja na mambo mengine, hivyo sioni taabu kupambana kwa ajili ya haki yangu.
"Ubaguzi wa rangi kwangu naona ni ujinga na unapoteza muda kufanya mambo makubwa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment