MUSSA Mgosi,
Kocha Msaidizi wa timu ya Vijana chini ya miaka 20 amesema kuwa kilichowaponza
Azam FC kushindwa kupenya mbele ya Simba ni safu ya mabeki kushindwa kusoma
alama za nyakati mapema pamoja na safu ya ushambuliaji kuwa na hofu.
Kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa Ngao ya Jamii, Simba ilishinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa 12 wa ngao
ya jamii uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mgosi amesema kuwa bado Azam FC ina nafasi ya
kurekebisha makosa yake kwa ajili ya michuano ya Kimataifa kwani muda upo.
“Nimeutazama
mchezo wa Simba dhidi ya Azam ulikuwa na ushindani mkubwa ila tatizo kubwa
linaonesha kwamba bado kuna tatizo la hofu kwa washambuliaji wa timu zetu
pamoja na mabeki kutokuwa makini kurekebisha makosa.
“Azam FC kwa
sasa wanapeperusha Bendera ya Taifa wana kazi ya kurekebisha makosa yao
waliyoyafanya ukizingatia wanashiriki michuano ya kimataifa hasa safu ya mabeki
pamoja na washambuliaji kwani walipata nafasi nyingi wakashikwa na hofu ya
kuzitumia,” amesema Mgosi.
Azam FC
itamenyana na Fasil Kenema ya Ethiopia mchezo wa marudio kati ya Jumamosi, Uwanja wa Chamazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment