August 21, 2019



FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Singida United kwa sasa anapata taabu kweli kusuka safu kali ya ushambuliaji kwani imekuwa ikisumbuliwa na ubutu huku safu yake ya ulinzi ikiruhusu mabao.

Kuelekea kwenye Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 24, tayari Singida United imecheza michezo ya kirafiki mitano na imeambulia kipigo kwa kukusanya jumla ya mabao 13 huku wao wakifunga jumla ya mabao manne.

 Matokeo yake yapo namna hii:- Singida United 0-1 Mashujaa, Singida United 0-4 Kagera Sugar, Singida United 1-3 Tanzania Prison, Singida United 2-3 Mbao, Singida United 1-2 Biashara United.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa huu ni mwanzo wa kukiandaa kikosi upya wana imani ya kufanya vizuri baada ya kugundua makosa.

“Kocha Minziro kwa sasa anapambana kusuka kikosi kipya ndio maana amekuwa akipata matokeo ambayo hayafurahishi, ila kwa sasa tayari benchi la ufundi limejua makosa ya timu kilichobaki ni kuyafanyia kazi,” amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic