KIKOSI cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo kimeanza mazoezi ya kujiaanda kwa ajili ya mchezo wa marudoio dhidi ya UD Songo ya Msumbiji.
Simba ina kibarua kizito kutafuta matokeo mbele ya UD Songo kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa hatua ya awali unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 Dar.
Mchezo wa kwanza ugenini Simba imelazimisha sare ya bila kufungana hivyo ili kusonga mbele ni lazima ipate ushindi ikiwa nyumbani.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa kikosi kitaonyesha namna uwanja wa nyumbani unavyopaswa kupewa heshima.
"Uwanja wa nyumabani una raha yake hasa ukiwa na mashabiki zako ni lazima uonyeshe kitu, mashabiki wa Simba utamaduni wetu tusiache lazima tuendeleze kwa manufaa ya nchi," amesema.
Kuhusu Simba,Brother Saleh naomba kuandika waraka wangu na hali ya mchezo nilivyoona wa Simba kati yake na UD songo kule Msumbiji.Waraka wangu mdogo katika kurasa hii ya maoni ya blog yako inawezekana kabisa usifike kunako macho ya viongozi wa Simba.Na hata ukifika pengine waisijali sana lakini kwangu mimi itakuwa nimetowa dukuduku langu la moyo kwakuwa nataka kuiona Simba mara hii inafika mbali zaidi na hakuna excuse au visingizio kwakuwa uongozi wa timu umejitoa na unajitoa kweli kweli kuhakikisha timu inajenga mazingira mazuri ya ushindi.Nianze kwa kusema nimeiangalia mechi ya simba na UD Songo na sikuhitaji kuwa na jicho la mwewe au jicho la tatu la ziada kuona mapungufu ya Simba kiasi cha kukaribia kuupasua moyo wangu.Simba ilicheza mchezo hovyo kabisa hasa katika eneo la ulinzi na nilichokibaini ni kwamba ubovu na udhaifu wa backline ya simba uliosababisha kubugizwa mabao kama mvua msimu uliopita ndio uliokuwepo kwenye mechi ya jumamosi dhidi ya UD Songo Mungu bariki fowardline ya UD Songo haikuwa makini licha ya kutengenezewa nafasi nyingi za wazi za kufunga na mabeki wa Simba. Kingine labda kilichosaidia ni uwepo wa Beno Kakolanya golini kwani mipira ile ya kushtukiza waliokuwa wakipiga golini washambuliaji wa UD Songo ndio magoli aliokuwa akifungwa Manula kirahisi na nadhani walikuwa wakidhani kuwa aliekuwepo golini ni Manula na hawakuwa wakijaribu kupiga mashuti yale kwa kubahatisha hapana walikuwa wakifuata maelekezo maalum kutokana na madhaifu ya kipa wa Simba waliyokuwa wakiyajua.Kubwa kuliko yote laiti kama Simba wangekutana na timu kama Nkana au As vita kwa mchezo Simba waliocheza juzi basi safari ya kuyaaga mashindano haya mapema ingekuwa imewadia. Msimu uliopita katika hatua za mtoano Nkana waliiotoa UD Songo kwa Mbinde na Simba wakaja kumtoa Nkana kwa Mbinde vile vile.kwa hivyo utaona UD Songo sio timu ya kubeza na moja ya hazina yao kubwa ni kwamba wapo fiti kweli kweli na Pumzi za ajabu licha yakuwa wana matatizo kidogo ya kiufundi. Ud Songo inaonekana wanafanya sana mazoezi ya mbio na mazoezi ya mbio ndio mazoezi mama ya soka.Kwa hivyo janga la kukosa kujiamini kwa timu ya Simba inapocheza ugenini halijatafutiwa dawa bado lipo pale pale na kwa kiasi fulani inanyongonyesha.Tuliwahi kuzungumza tatizo la kocha wa Simba la yeye mwenyewe binafsi kukosa kujiamini anapokuwa nje ya Daresalam hasa kwenye mechi za kimataifa kitu ambacho huwaathiri wachezaji wake pia. Tatizo jengine la kocha wa Simba ambalo bado hajalifanyia kazi ni kuchelewa kufanya mabadiliko ya haraka na ya kufaa pale inapotokezea mchezaji fulani anacheza chini ya kiwango uwanjani. Simba sasa ina kikosi kipana na wachezaji wenye uwezo hasa, licha yakuwa wageni lakini sio wageni wa mpira ni mchecheto wa kocha mwenyewe kukosa kuwaamini. Mtu kama Deo Kanda amecheza Champion ligi na Mazembe msimu uliopita na alikuwa moto kwanini kocha anashindwa kumuamini? Tatizo jengine la kocha wa simba ni kung'ang'ania baadhi ya wachezaji hata kama hawapo kunako ubora. Msimu uliopita tuliona kombanisheni ya Dilunga na chama ilivyowanusuru Simba.
ReplyDeleteBoko hivi sasa ni wa kukaa benchi apumnzike kidogo labda amechoka kwani kapoteza ubora wake. Nilitarajia uongozi wa Simba hautosubiri mpaka timu inatupwa nje ya mashindano ndio waitishe kikao? Hizi mechi za mtoano ni hatari zaidi huwezi kutegemea mechi za nyumbani tu. Tuliona goli moja la ugenini zidi ya Nakana lilivyoivusha Simba kuingia hatua ya makundi. Hii tabia ya simba kujilegeza ugenini ipo siku itawatumbukia nyongo. Kama ni vipi basi bora timu iajiri kocha maalum wa mabeki kwani kocha anaonekana kuwa na mapungufu makubwa kwenye eneo hilo.Timu yenye viungo nane fundi vipi inashindwa kumiliki mpira kama vile tulivyoona kule Msumbiji? Ni matarajio yetu kuona uongozi unakaa na kocha kabla mambo hayaja haribika. Kocha anatakiwa kuonesha mabadiliko ya mchezo katika mechi za ugenini la sivyo hata wapinzani wa Simba walishajua yakuwa ukitaka kuitoa Simba basi ni kuifunga Daresalam na hakuna kisichowezekana kwani ugenini ni nyanya si la hasha UD Songo wakaja kuitoa Simba nishai hapa hapa Dar.
Umeongea vema mkuu.. naomba uongozi wa simba ulione hilo. Kocha naona anataka kuleta mambo ya amunike..mchezaji kama Bocco kachemka anazunguka tuu uwanjani..kwann usiingize hata viungo wote ubakishe mshambuliaji mmoja mbele.Mabadiliko yawe yanafanywa mapema mtu game inapomkataa sio mpaka majanga yatufike tuanze tena mambo ya jasho na damu.
ReplyDelete