KAZI kubwa
imebaki kwa timu ya Taifa ya Tanzania kupata matokeo mbele ya Kenya nchini
Kenya kwenye mchezo wa marudio ya kufuzu kupata nafasi kushiriki michuano ya
Chan.
Matarajio ya
awali ilikuwa ni kuona timu inapata matokeo kwenye mchezo wa kwanza nyumbani
kisha safari ya Kenya hesabu zilikuwa ni kwenda kukamilisha ratiba.
Mwisho wa
siku kinachotokea ndicho tunachokipokea kwani Mungu anapanga na binadamu
anapanga pia ni matokeo yetu tunayachukua na kuyafanyia kazi.
Kumaliza
dakika 90 bila kufunga bao nyumbani ni matokeo ambayo kwa kiasi fulani
yanawavunja moyo watanzania kwa kushusha ile imani yao kwa timu ya Taifa.
Ila bado
ninaona kuna nafasi ya kupata matokeo ugenini pia licha ya kushindwa kufanya
vizuri nyumbani mchezo wa kwanza.
Tusisahau
kwamba kambi ya timu ya Taifa imeundwa kwa muda mfupi na matokeo tumeyaona
namna wachezaji walivyojituma kwa juhudi na kwa bidii kusaka ushindi.
Mwisho wa
siku tunaona kwamba sare imetuweka hapa na tunaanza safari nyingine kuifuata
Kenya kwa ajili ya kupambana zaidi.
Kwenye
maisha ya soka hakuna ambacho kinashindikana na hakuna ruhusa ya kukata tamaa
licha ya ushindani kuwa mkubwa kikubwa ni kuungana.
Wachezaji
wanajua namna walivyopambana na makubaliano ya kusaka ushindi ndani ya ardhi ya
nyumbani hivyo kushindwa kutimiza hesabu za mwanzo maana yake kazi mpya
inaongezeka.
Kwa sasa
watanzania wanapaswa waendeleze ule muungano na ushirikiano kwani kazi bado
inaendelea na hakuna ambaye amemaliza safari ndo kwanza mgawanyiko wa kwanza
umekwisha.
Dakika 90 za
kwanza zimekamiilika zimebaki dakika 90 nyingine za ugenini ambazo zitakuwa ni
za machozi na damu katika kutafuta ushindi bado nafasi ipo.
Uwezekano wa
kutimiza lile lengo la Taifa kufuzu michuano ya Chan bado ipo mikononi mwa
wachezaji wenyewe ndani ya uwanja.
Kilichobaki
ni kwa mashabiki kuipa sapoti timu ya Taifa licha ya kuona kwamba imeshindwa
kupata matokeo.
Kuikatia
tamaa sio jambo jema kwani linaimaliza moja kwa moja timu yetu ya Taifa ambayo
kwa sasa haipo sehemu mbaya kupata matokeo.
Wao wameweza
kulazimisha sare nyumbani kwetu basi nasi pia tuna nafasi ya kulazimisha kupata
matokeo nyumbani kwao jambo litakaloongeza furaha ya kweli.
Matokeo
ambayo yametokea hatuna uwezo wa kuyabadili kwa sasa zaidi ya kujipanga upya
kwenda kumaliza kazi ambayo tumeianza na kwa juhudi kubwa.
Mashabiki
wengi waliojitokeza uwanja wa Taifa ni jambo la uzalendo hivyo ndivyo inatakiwa
kuwa siku zote mshikamano ni kitu cha msingi yanapofika
masuala ya kupambana
kwa ajili ya Taifa.
Vijana
wamekaa muda mfupi na wameweza kupambana kwa kiasi kile imani kubwa ni kwamba
kama wakipata nafasi nyingine ya kuaminiwa lazima wataitumia vizuri.
Mashabiki
msiwavunje moyo vijana kwa kuwa safari bado inaendelea na wahenga walisema kuwa
kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi .
Bado kwa
sasa kuna nafasi ya kufanya vema na kupenya mpaka Cameroon mwaka 2020 kushiriki
michuano ya Chan ni suala la kusubiri muda na kuendelea kutoa sapoti katika
kila jambo.
Taifa letu
la Tanzania lina vipaji vingi na wengi wanajua kucheza mpira hivyo ni suala la
kusubiri na kuona.
Makosa ya
vijana ni sehemu ya mpira hasa ukizingatia kwamba kwa sasa tunakwenda kucheza
tukiwa hatuna presha kubw kama ilivyokuwa mwanzo.
Presha
ilikuwa kubwa kwa kuwa tulikuwa nyumbani na kila mmoja matarajio yake ilikuwa
kuona tunashinda tena kwa idadi kubwa ya mabao.
Moja ya
sehemu ya matokeo kwenye mpira ukiachana na kushinda ama kupoteza na sare pia
ni aina ya matokeo japo si matokeo yanayopendwa sana na mashabiki pamoja na
benchi la ufundi.
Mwalimu
yoyote yule duniani anapopeleka timu uwanjani hesabu zake ni kuona timu inapata
matokeo chanya ambayo ni ushindi.
Rai yangu
kwa watanzania wote kwa sasa kushikamana na kuungana kwa ajili ya kuiombea timu
yetu ya Taifa ikafanye vizuri kwenye mchezo wa marudio ambao utafanyika nchini
Kenya.
Agosti 4 sio
mbali na siku zinakwenda kasi hivyo mashabiki tuendelee kuwa mstari wa mbele
kuipa sapoti timu yetu ambayo inapambana kupeperusha Bendera ya Taifa.
Muda wetu wa
kufikia mafanikio kwa sasa ni kwenye mchezo wetu wa marudio na tuna imani
nafasi ya kufanya vizuri ipo na inawezekana kabisa.
Jambo la
msingi ni kuona sasa namna gani tunaweza kujipanga upya hasa kwa kufanyia kazi
yale makosa ambayo tumeyafanya mchezo wa kwanza.
Mchezo wa
pili utakuwa na ushindani na kila mmoja anahitaji matokeo ila haimaanishi kwamba itakuwa kazi nyepesi kupata matokeo
kikubwa ni imani na kupambana kutafuta matokeo.
Furaha ya
watanzania kwa sasa ipo mikononi mwa wachezaji ambao jukumu lao ni kupambana
kupata matokeo chanya.
Mashabiki wapeni
sapoti vijana wetu wa timu ya Taifa kama ambavyo mmefanya kwenye mchezo wa
kwanza.
Pana kosa hapo juu la mwandishi inafaa lisahihishwe. Sio Mungu anapanga na binaadamu anapangua Kwa sababu Mungu akishapanga Hakuna binaadamu yeyote mwenye uwezo wa kupangua Amri yake. Sahihi Ni binaadamu anapanga na Mungu anapanguwa.
ReplyDelete