BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' amesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi ni kujiamini na wachezaji kufuata mbinu.
Jana Tanzanite, ilifungua pazia kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini na ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.
"Kazi ya kwanza haikuwa nyepesi na tulianza kwa hofu licha ya kujituma ila mwisho wa siku tuliyazoea mazingira na kila mmoja akawa na morali kubwa ya kushinda.
"Ni mwanzo mzuri kwetu hivyo tuna imani ya kuendelea kufanya vema katika michezo yetu yote kwani siri ya ushindi ipo kwenye kujiamini na kujituma," amesema.
Diana Msemwa nyota wa Tanzanite alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kwenye mchezo huo dhidi ya Botswana uliochezwa Uwanja wa Gelvalande,Port Elizabeth, Afrika Kusini.

0 COMMENTS:
Post a Comment