LIVE!! KIPINDI CHA PILI: SIMBA 3-1 JKT TANZANIA, MECHI YA LIGI KUU BARA
FULL TIME; SIMBA SC 3-1 JKT TANZANIA
Dak ya 90+2, JKT wameamka kwa kasi, na mpira umekwisha.
Dak ya 90+1, Ajibu anapoteza mpira kizembe na kuifanya Simba ikose bao kirahisi.
Dak ya 90+1, faulo kuelekezwa Simba, anaonekana Shiboub akiwa na mpira
Dak ya 90, dakika tatu za ziada zimeongezwa.
Dak ya 86, Fraga anaanza mpira nyuma, anapasia kati mwa uwanja lakini JKT wanaunyaka, piga pale kwake Songo, goooooli, JKT wanapata bao la kwanza kupitia kwa Songo.
Dak ya 85, Fraga amepewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Aziz.
Dak ya 84, mchezaji Jabir Aziz ameanguka chini baada ya kuumia goti, mpora umesimama.
Dak ya 83, Mpaka sasa Simba wameotea mara mbili wakati JKT hawajaotea hata mara moja.
Dak ya 82, golikiki, mpira unapigwa kuelekea JKT
Dak ya 79, faulo wanapata JKT, inapigwa lakini inaokolewa na mabeki Simba
Dak ya 77, umakini umekuwa shida katika eneo la ushambuliaji, wanashindwa tena kutumia nafasi vema.
Dak ya 73, Simba wanapasiana kati mwa uwanja wakijaribu kupata mwanya wa kupata nafasi ya kufunga, piga krosi kwake Miraji Athumani, goooli, anafunga la pili.
Dak ya 72, kona ninapigwa kuelekea JKT, inaokolewa.
Dak ya 70, mpira unarushwa kuelekea JKT baada ya kuutoa nje.
Dak ya 69, JKT wanaanza upya langoni kwao, wamekuwa wakipata nafasi za hapa na pale lakini kufunga imekuwa ngumu.
Dak ya 65, faulo inapigwa kuelekea JKT, ni nje kidogo ya 18, wanafanya mipango mizuri ya kupiga lakini mpira unatoka nje.
Dak ya 65, Kagereee, piga shuti kali, linagonga mwamba na kurudi ndani.
Dak ya 64, nafasi nyingine kwa JKT kupata bao lakini umakini unakosekana,
Dak ya 63, kona inapigwa kuelekea Simba, inapigwa lakini inaokolewa kwa kichwa.
Dak ya 62, Hassan Dilunga anakosa kufunga bao baada ya kupata nafasi nzuri,
Dak ya 58, Goooooli, Kagere anaandika bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.
Dak ya 56, Simba bado wanahaha kupenya ngome ya JKT.
Dak ya 55, faulo nyingine kuelekea JKT, bado kuta zote kwa timu mbili zimekuwa ngumu kupitika.
Dak ya 53, kadi ya njano inaenda kwa Madenge Ramadhan baada ya kumfanyia faulo Dilunga.
Dak ya 52, JKT wamefanya shambulio moja lakini umakini kwa washambuliaje wake umekosekana.
Dak ya 51, hatari nyingine eneo la JKT, mpira uanenda kwake Mzamiru, unaokolewa.
Dak ya 49, Simba wamekosa kutumia nafasi vema ya kuandika bao la pili, ni baada ya beki JKT kuzubaa.
Dak ya 45, kipindi cha pili kimeshaanza
HALF TIME: SIMBA SC 1-0 JKT TANZANIA
Dak ya 45+1, kosakosa imetokea langoni mwa JKT
Dak ya 45, dakika moja ya ziada imeongezwa.
Dak ya 43, kona wanapata Simba, inapigwa lakini inakuwa goli kiki.
Dak ya 41, kuta zote zimekuwa ngumu kupitika, zimesalia dakika tano mpira kumalizika.
Dak ya 38, Haruna Shamte anapewa kadi ya njano kw akucheza madhambi.
Dak ya 37, Simba wanakosa bao la pili, ilipigiwa kichwa na Kagere lakini beki JKT anaokoa mpira.
Dak ya 32, Simba wanazidi kumiliki soka zaidi ya JKT, wakitafuta bao la kuongeza.
Dak ya 29, kona ishapigwa, goli kiki.
Dak ya 28, faulo inapigwa kuelekezwa JKT, anapiga Chama, inakuwa kona.
Dak ya 26, JKT wameonekana kuwa wagumu eneo la ulinzi, wanawapa wakati mgumu Simba kupenya licha ya kuwa nyuma kwa bao 1-0.
Dak ya 25, Chama anafanyiwa madhambi, gozi linapigwa kuelekea JKT
Dak ya 23, JKT wanapata faulo kushoto mwa uwanja nje ya 18, imepigwa lakini Manula anadaka.
Dak ya 22, Simba wanapasiana kuelekea langoni mwa JKT, mabeki JKT wanaokoa.
Dak ya 21, nafasi nyingine kwa JKT, pigwa shuti kali pale, Manula anadaka.
Dak ya 20, Manula ameodondoka chini baada ya kugongana na mchezaji JKT, mpira umesimama, ushaanza.
Dak ya 19, hatari langoni mwa Simba, pigwa kichwa pale, inaokolewa.
Dak ya 18, faulo kuelekezwa Simba
Dak ya 17, JKT wamekuwa wakiganya mashambulizi ya kushitukiza, japo hali imekuwa ngumu kupata bao.
Dak ya 16, kona kuelekezwa JKT, wanapiga Simba, tayari ishapigwa na inaokolewa na mabeki JKT
Dak ya 15, JKT wanapata nafasi nzuri ya kuandika bao la kusawazisha lakini wanakosa umakini, Manula anadaka kiulaini.
Dak ya 14, shambulizi lingine wanafanya Simba lakini linashindwa kuzaa matunda.
Dak ya 12, mchezaji JKT anatoa mpira nje na unarushwa kuelekea Simba, tayari usharushwa.
Dak 13, tayari JKT wameshaanza, wana mpira eneo lao la ulinzi.
Dak ya 12, faulo inapigwa kuelekezwa Simba baada ya mchezaji JKT kuchezewa madhambi.
Dak ya 11, Manula anarudishiwa mpira nyuma ili kuanza mchezp upya.
Dak ya 11, Simba wanapasiana eneo la kati mwa uwanja wakionekana wana dhamira ya kusaka bao la pili.
Dak ya 10, Chama anafanyiwa madhambi na mpira unaelekezwa JKT
Dak ya 9, kona ya kwanza inapigwa kuelekezwa Simba, imepigwa lakini inakuwa faulo.
Dak ya 8, JKT wanajaribu kufanya shambulio moja lakini ukuta wa Simba unakuwa imara.
Dak ya 5, Simba wameanza kwa mashambulizi makali dakika hizi za mwanzo.
Dak ya 1, Meddie Kagere anaipatia Simba bao la kwanza
Wenye ligi yao wamerudi this is simba hao kandambili hawana chao
ReplyDeleteTunasubiri watolewe za zesko warudi kwenye matope jangwani
ReplyDeleteMambo yanaanza hayo na wale jamaa wamepigwa bumbuwazi na kuanza kuvunjika moyo mapema na huku wakiwa wamejiinamia. Hakika Mnyama kaanaza kunguruma mapema.
ReplyDeleteThis is the Simba next level.Mwaka huu ubingwa ni round ya kwanza tuu tayari Simba bingwa
ReplyDeleteSIMBA ongezeni umakini zaidi ktk kufunga magoli maana nafasi nyingi mnatengeneza lkn tunashindwa kuelewa kwa nini mnashindwa kufunga magoli.Kweli tuwalaumu makocha kwa uzembe huu na hii kila mechi inajitokeza na ukweli hata ukiangalia takwimu za nyuma za michezo ya Simba inakuwa inamiliki (possesion) zaidi mpira na hata mechi ya UD Songo Simba alikuwa na possesion ya 64% dhidi ya wapinzani wao 36%.Na leo tena Simba imerudi na makosa hayo hayo ya kutokuwa makini ya kutumbukiza magoli kwenye nyavu.Hii itawawia ngumu sana kwa mechi zijazo maana timu nyingi zinaisoma madhaifu ya Simba na hasa kutumia mtindo wa kupaki basi kama tulivyoona ligi iliyopita.Wakikuwahi kwa goli moja la kubahatisha ndio basi tena inakuwa taabu kulirudisha.Mpira wa soka ni magoli.
ReplyDelete