UONGOZI wa
Mtibwa Sugar umesema kuwa hautakuwa na cha msalie mtume mbele ya Lipuli kwenye mchezo wa leo utakaochezwa uwanja wa Samora.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa
wamefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya msimu mpya na hesabu zao ni kushinda ugenini.
“Msimu
uliopita hesabu zetu ziligoma baada ya kuteleza kidogo mwanzo ila kwa sasa
tumeshajifunza na kazi inaanza rasimi mbele ya Lipuli mpaka ligi inaisha
tutakuwa pale tunapohitaji, tunawapiga wakiwa kwao” amesema Kifaru.
Msimu
uliopita Mtibwa ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 38
na ilijikusanyia pointi 50, leo itafungua pazia kwa kuanza na Lipuli uwanja wa
Samora itamkosa nahodha wao Shaban Nditi ambaye ni majeruhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment