SIMBA KUSHUSHA SAPRAZI LEO
Yanga jana imechezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting ikiwa ni mechi ya kwanza ya ligi kuu lakini upande wa pili yaani Simba, kocha wao Mbelgiji, Patrick Aussems ametamba watashusha bonge la saprazi leo Alhamisi.
Aussems amesisitiza kwamba baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hasira zote wanazihamishia kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la FA na watashusha vipigo vya kushtua.
Katika mechi ya leo watakayocheza dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru huku akiwaomba mashabiki wasiwatenge kutokana na matokeo ya wikiendi iliyopita. Akizungumza na Spoti Xtra, mara baada ya mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Gymkhana, Aussems alisema wamejipanga kisaikolojia na watapambana.
“Nawaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono katika ligi na Kombe la FA baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. “Hayakuwa malengo yetu kuondolewa katika hatua hii, bahati haikuwa yetu kwani timu ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tulishindwa kuzitumia, ”alisema kocha huyo ambaye Mei 26, mwaka huu aliongeza mkataba wa mwaka mmoja na Simba.
“Hivyo, tunarudi kwenye ligi na kikubwa mashabiki waendelee kujitokeza uwanjani kama mwanzoni kwa ajili ya kutupa sapoti ili tufanikishe malengo yetu.
“Kuna vitu vingi tumejifunza baada ya kuondolewa Caf, katika mchezo huo na Songo tulifanya makosa katika dakika 20 za mwanzo ambazo tuliruhusu bao nyumbani, hivyo akili na nguvu zetu tunazihamishia kwenye ligi na Kombe la FA na kikubwa kuchukua makombe yote,” alisema Aussems ambaye moja ya malengo aliyopewa na bodi ya Simba ni kutetea ubingwa wa Tanzania na kufi ka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment